SHEHE wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu akizungumza wakati wa kikao hicho kulia Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa Tanga Askofu Dr Jotham
Mwakimage
SHEHE wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu akizungumza wakati wa kikao hicho kulia Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa Tanga Askofu Dr Jotham
Mwakimage
Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa Tanga Askofu Mstaafu wqa Kanisa la TAG Dr Jotham Mwakimwage |
Kamanda wa polisi Mkoa wa
Tanga Blasius Chatanda kulia akifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho
FR
Richard Kimbu wa Kanisa Katoliki Mkoa wa Tanga akichangia jambo kwenye
mkutano huo kushoto ni FR Severine Msigiti wa RC Tanga na kulia ni Fr
Martin Maganga wa Kanisa Katoliki Mtakatifu Theresia Tanga
MCHUNGAJI wa Kanisa la Waadiventist Wasabato lililopo Kana Jijini Tanga, Jackson Mdingi akichangia jambo wakati wa kikao hicho kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Tanga Shehe Juma Bakari
Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Tanga Shehe Juma Bakari akisistiza jambo wakati wa kikao hicho
KUELEKEA
Uchaguzi Mkuu Octoba 28 mwaka huu kamati ya viongozi wa dini mkoani Tanga
wamekutana huku wakitoa maazimio matano ikiwemo kupinga aina yoyote ya vurugu
na maandamano, viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza wakati wa
uchaguzi huo
Akisoma
maazimio ya Baraza la Amani mkoa wa Tanga Askofu Mstaafu wa Kanisa la TAG Dkt
Jonson Mwakimwage wakati wa kikao cha Baraza hilo ambacho kiliketi kwenye
ukumbi wa Tanga Beach Jijiji Tanga.
Alisema
wao kama viongozi wa dini hawatakubali kuona vurugu na maandamano yakitokea wakati
wa uchaguzi huo badala yake watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vitendo vya
namna hiyo havitokei kwenye jamii ili watanzania waweze kushiriki kwa amani
kwenye uchaguzi huo
“Leo
viongozi wa dini mkoani Tanga tumekutana kwenye kikao hiki maalumu kuelekea
kwenye uchaguzi mkuu lakini moja ya maazimio yetu ni kutaka uchaguzi kufanyika
kwa amani na tunakataa maandamano ya vurugu ya aina yoytote”Alisema Askofu
Mwakimage.
Alisema
wao kama baraza hilo wanakataa na kutokuuunga mkono vitendo vya maandamano na
vurugu aina yoyote ikiwemo viashiria vya matamshi vinavyoashiria uvunjifu wa
amani hawavikubaki
Askofu
huyo alisema kwamba wao kama kamati ya amani mkoa wameyakataa na hawataridhia watu
wenye matamshi mabaya ya kuvuruga amani wakati wa uchaguzi huo huku wakieleza watakaochaguliwa
watakubaliana nao na kuwaunga mkono
Awali akizungumza wakati wa kikao hicho Shehe
wa Mkoa wa Tanga Juma Luwuchu alisema wao viongozi wa dini wana kazi kubwa ya
kuhakikisha waanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhimizxa amani,
Alisema
kwamba moto mkubwa mkubwa chanzo chake ni cheche hivyo wakichezea cheche ya
moto wananchi kwa sababu uchaguzi ni siku moja na maisha ni kile siku hivyo
walitambue hilo na kufikiria.
“Ndugu
zangu tusichezee cheche wakati wa uchaguzi kwani siku moja tukichezea tunaweza
kufanya tusiwe na nyumba ya kuwaongoza watu misikitini wala makanisani”Alisema
Shehe Luwuchu.
Aliwataka
viongozi wa dini wasigeuke kuwa wapembe wa wanasiasa badala yake wahakikisha
wanatumia nafasi zao kuendelea kuihubiri amani na utulivu uliopo hapa nchini
“leo
kumejitokeza baadhi ya viongozi wanaojiita ni wa dini wanatamka waziwazi na
kutamka baadhi ya vyama kwamba hivi ndio vyama na kuhamasisha vijana kujitokeza
barabarani hiyo sio dini yetu inavyoelekeza huku wengine wakisema baada ya kura
waendelee kukaa vituoni huo sio utaratibu wa dini”Alisema
KamaKamanda wa polisi Mkoa wa
Tanga Blasius Chatanda ameonya watu au Kikundi Cha watu
ambacho kitajaribu kufanya uvunjifu wa amani katika uchaguzi Mkuu ujao kuwa
watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kauli hiyo aliitoa wakati akiongea
na waandishi wa habari kuhusu mikakati iliyowekwa na Jeshi hilo kuelekea katika
zoezi la uchaguzi Mkuu.
Alisema Kuwa Jeshi hilo limejipanga
kuhakikisha zoezi la upigaji Kura hadi kutangazwa kwa matokeo linakuwa la
salama na amani.
“Niwaambie waliotakaojaribu
kuingia mitaani na kufanya maandamano Basi niwaambie watakiona kitakacho
watokea kwani tumejipanga kweli kweli safari hii”alisema RPC Chatanda.
Aidha aliwataka wananchi kuendelea
kutoa taarifa za kuwepo vitendo vya viashiria vya uvunjifu wa amani katika
maeneo mbalimbali ili viweze kudhibiti mapema kabla hazijaweza kuleta athari.
“Tuwaache watu watimize
majukumu yao ya kikatiba kwa amani na utulivu na Wala wasiogope kwenda kupiga
kura kwani ulinzi umeimarishwa na kitakuwa na Hali yausalama siku
hiyo”alisema Chatanda