Home Mchanganyiko EXAUD KIGAHE AAHIDI NEEMA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

EXAUD KIGAHE AAHIDI NEEMA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

0

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za neema wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa ahadi za nane kwa wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge wao.

Na Fredy Mgunda,Mufindi Kaskazini.

 

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo
la Mufindi Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe ametoa
ahadi za nane kwa wananchi wa jimbo hilo kama watampatia ridhaa ya kuwa mbunge
wao.

Akizungumza wakati wa kufunga
kamapeni za kuomba kura kwa wananchi wa jimbo la Mufindi,Exaud Kigahe alisema
kuwa jimbo la Mufindi Kaskazini linakabiriwa na changamoto ya miundombinu ya
Barabara ambazo zimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima hivyo akipewa ridhaa ya
kuwa mbunge atahakikisha anatatua kero hiyo.

Alisema kuwa atahakikisha
anaboresha sekta ya Elimu kwa kujenga na kukarabati majengo ya
shule,kuanzisha  mashindano ya kumpata mwananfunzi bora na mwalimu
bora kwa atakayefanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanafunzi kufaulu kwa wastani
mzuri.

“Wananchi wa jimbo la
Mufindi wengi ni wakulima hivyo siwezi kuisahau sekta ya kilimo kwa kuwa hata
mimi nimekulia kwenye family ya wakulima hivyo nitahakikisha kuwa tunaboresha
masoko ya wakuliwa ili waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri” alisema Kigahe

Aidha
Kigahe alisema kuwa ahadi nyingine ni pamoja na 
viwanda,afya,biashara,umeme
na michezo ambazo atazifanyia kazi kama akiwa mbunge wa jimbo la Mufindi
Kaskazini.

 

“Kazi
kubwa mliyonipa nitaifanya kwa nguvu na niwahakikishie sisi wabunge watatu wa
Wilaya ya Mufindi (Kihenzile na Chumi) tutafanya kazi kwa pamoja kwa
kuwa  lengo kubwa ni kuleta maendeleo”alisema  Kigahe

 

 

 

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa Dr Abel Nyamahanga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi kwenye kufunga kampeni
hizo aliwaomba wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuhakikisha wanampa kura
nyingi Mgombea Ubunge Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe kwa kuwa ameamini na Rais.