Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,John Shibuda,akizungumza na waandishi wa habariJijini Dodoma kuhusu kuwaasa na kuwashauri wagombea wa nafasi mbalimbali wa Tanzania na Zanzibar kuwa wawe tayari kupokea matokeo hayo.
…………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini,John Shibuda amewaasa wagombea wa nafasi mbalimbali za Urais, ubunge na udiwani kujiandaa kisaikolojia na kuwa na fikra tulivu za utayari wa kupokea matokeo ya kushinda au kushindwa katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28,mwaka huu.
Shibuda ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwaasa na kuwashauri wagombea wa nafasi mbalimbali wa Tanzania na Zanzibar kuwa wawe tayari kupokea matokeo hayo.
Shibuda amesema kuwa uchaguzi ni fumbo la kiini macho la siasa za uzimuaji wa hamasa za vuguvugu za kushindania hisia na kushindania imani za wapiga kura.
“ Kwa sasa tupo katika kipindi cha lala salama, ni kipindi cha kukaririsha wananchi nguvu za hoja za ukweli halisi ama kukaririsha wananchi hoja za nguvu za uongo mtamu na za ukweli bandia.”amesema Shibuda
Shibuda amesema kuwa ameamua kutoa ushauri kwa wagombea na kwa wapiga kura ili kila mdau muomba kura za wapiga kura kujiweka sawa kwa kuwa na uimara kwa maamuzi ya kupatikana uongozi bora wa kuendeleza ustawi na maendeleo ya jamii,uchumi na Taifa letu.
“ Hivyo nitoe wito kwa kila mgombea ajiandae kisaikolojia na kwa moyo mkujufu awe tayari kupokea matokeo ya ushindi au ya kushindwa, kila mgombea akubali somo la kuwa asiyekubali kushindwa siyo msindani, na kuunjika kwa jembe siyo mwisho wa uhunzi”amesisitiza Shibuda.
Shibuda amesema kuwa kama Tanzania ingekuwa inachangua kaptani wa timu ya mpira anauhakika kura nyingi zingekwenda kwa John Magufuli ikiwa na sawa na kuchaguliwa kwa Messi au Ronaldo ili kuongoza morali na kuongoza ari ya timu zipate ushindi kwa manufaa ya klabu zao.
Hata hivyo amewakumbusha wagombea na mashabiki wa vyama vya saisa kuwa ushindi hautokani na taswira ya hadhara zilivyokuwa katika mikutano ya kampeni.
“ Nipenda kusema kuwa busara za wanasiasa na za mashabiki wa vyama vyote ya kuwa, kura za ushindi kwa kila mshindi hazitatokana na kigezo cha taswira ya hadhara zilivyokuwa katika vipindi vya mwitikio wa mahudhurio ya wasikilizaji wa kampeni”amesema Shibuda
Shibuda ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama cha TADEA, amesema umma hautoi kura kwa siasa za mtu muongo anayesema anauwezo wa kuona gizani paka mwesi aliyefumba macho na kuwaogopa wagombea wavaa siasa umiza madai ya wahanga wapigania uhuru wa jamii na Taifa..
Hivyo kura zitaenda kwa mtu ambaye amegusa hisia za umma na anayekonga mioyo ya umma kutokana na kauli zake kwa wananchi.Wapiga kura huchagua kiongozi mwenye sifa za uzalendo kwa kulinda rasilimali za Taifa.