Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Babati mkoani Manyara katika Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa leo Jumapili Oktoba 25, 2020.
Rais Dk. Magufuli amewapongeza wananchi wa Babati kwa kumpitisha bila kupigwa mbunge mteule wa jimbo hilo Pauline Gekur ambaye awali alikuwa ni mbunge wa CHADEMA.
Katika Hatua nyingine Rais Dk. Magufuli amemuagiza Waziri wa Nishati Dk. Meldard Kalemani kuhakikisha analeta wataalamu wa Tanesco kuanzia kesho Jumatatu Oktoba 26, 2020 kuhakikisha wanakamilisha uunganishaji wa umeme kwa wananchi 400 ambao wamelipia kuunganishiwa umeme katika wilaya ya Babati lakini bado hawajaunganishwa.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-BABATI)
Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Babati mkoani Manyara katika Mkutano wa Kampeni za CCM leo Jumapili Oktoba 25, 2020.
Kutoka kulia ni Waziri Mkuu mstaafu Mzee Fedrick Sumaye, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara Ndugu Rodrick Mpogolo na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole wakipiga makofi wakati wimbo ukitumbuizwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ali Kakurwa na baadhi ya wagombea ubunge wa mkoa wa Manyara kushoto ni Mbunge mteule wa jimbo la Babati Pauline Gekur.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ali Kakurwa akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Kwaraa mjini babati.
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Fedrick Sumaye akizungumza nakumuombea kura mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Fedrick Sumaye akiwa ameketi na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Rodrick Mpogolo wakishiriki katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika mjini babati.
Baadhi ya viongozi mbalimbali na watu maarufu wakiwa katika mkutano huo wa kampeni.
Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali wakishiriki katika mkutano huo kwa ajili ya kuombea mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionesha maelfu ya wananchi wakiwa wanamsikiliza mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati.