Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Bomang’ombe wilayani Hai mmkoani Kilimanjaro leo Jumatano Oktoba 21,2020.
Rais Dk Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura kwa wingi itakapofika Oktoba 28 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Baadhi ya wananchi wamesikika wakisema Kando ya Mkutano huo wakisema “Hakuna namna kura zetu tupeni Rais Magufuli tu aliyoyafanya kwetu wana Hai na nchi kwa ujumla anastahili zawadi ya kura”
(PICHA NA JOHN BUKUKU-BOMANG’OMBE-HAI)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akiwahutubia wananchi wa Bomang’ombe wilayani Hai mmkoani Kilimanjaro leo Jumatano Oktoba 21,2020.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Hai Saasisha Mafue akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye mkutano wakampeni uliofanyika Bomang’ombe mjini Hai leo.
Kulia ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Mwanga Ndugu Tadayo, Kanali Ngemela Lubinga Katibu wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kiamataifa CCM na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole.
Mwenyekiti wa CCM mkoawa Kiliamanjaro Patrick Boisafi akimkaribisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli
Mgombea Ubunge wa jimbo la Hai Saasisha Mafue akimuombea kura Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika mkutano huo kwa ajili ya kuombea mkutano huo.
Wagombea udiwani na baadhi ya viongozi wa CCM wakiwa jukwaa kuu katika mkutano huo uliofanyika Bomang’ombe mjini Hai.
Viongozi wa dini ya Kiislamu wakiomba dua katika mkutano huo.
Bango kubwa likihamasisha kumpigia kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Baadhi ya picha mbalimbali zikionesha wananchi mbalimbali wakiwa wamejotkeza kwenye uwanja wa Bomang’ombe mjini Hai ili kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli.