TIMU ya Pyramids ya Misri jana wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Horoya AC ya Guinea mabao ya Ibrahim Hassan dakika ya 74 na Abdalla El Said dakika ya 75 katika mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco.
Sasa Pyramids itakutana na RSB Berkane ambayo juzi iliitoa Hassania Agadir, zote za Morocco kwa kuwachapa 2-1 Uwanja wa Prince Moulay Abdallah Jijini Rabat na kutinga fainali kwa mara ya pili mfululizo.
Berkane ambayo ilifungwa na Zamalek kwa penalti kwenye fainali ya msimu uliopita, mabao yake yalifungwa na Nahodha, Mohammed Aziz yote kwa penalti dakika ya 20 na 61.

Bao pekee la Hassania Agadir ambayo juzi ilipoteza mechi ya kwanza kati ya 12 za Kombe la Shirikisho msimu huu, lilifungwa na Imad Kimaoui dakika ya 30.
Fainali itachezwa Jumapili Uwanja wa Prince Moulay Abdallah, Rabat kuanzia Saa 5:00 usiku.