Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga mrema aliyefika eneo la Himo pamoja na wanachama wachama chake ili kumlaki leo Jumatano Oktoba 21,2020.
Akizungumza mara baada ya Rais kumpa nafasi ya kumuombea kura Mrema amewaambia watu wa Himo na Vunjo kuwa kura zote kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli na ubunge kura ziende kwa Dk. Charles Kimei.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-HIMO-KILIMANJARO)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga mrema aliyefika eneo la Himo pamoja na wanachama wachama chake ili kumlaki leo Jumatano Oktoba 21,2020.
Mzee Agustino Lyatonga mrema pia alileta mbuzi mkubwa pamoja na mkungu wandizi kwaajili ya zawadi ya Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mweyekiti wa Chama cha TLP akielekea kwenda kumsalimia Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati wanachama wa chama hicho waliposhiriki katika mapokezi ya Mh. Rais.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Mzee Agustino Lyatonga Mrema akiwa pamoja na wanachama wenzake wakimsubiri Rais Dk. John Pombe Magufuli eneo la Himo mkoani Kilimanjaro.