Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Eneo la Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga baada ya kuwasili mkoani humo akitokea mkoani Dar es salaam na Pwani leo Jumatatu Oktoba 19,2020.
(PICHA NA JOHN BUKUKU -MKATA-TANGA)
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Tanga waliojitokeza kumlaki Rais Dk John Pombe Magufuli alipowasili mkoani Tanga akitokea jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Ndugu Hebry Shekifu akimkaribisha Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk John Pombe Magufuli kuzungumza na wananchi wa Mkata mkoani Tanga.
Maelfu ya wananchi wakiwa wamejitokeza kumlaki mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Rais Dk John Pombe Magufuli eneo la Mkata wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.