*****************************************
Baada ya uzinduzi wa simu mpya ya Infinix HOT 10 sasa Infinix imekuja na promotion ya Infinix TUPO LIVE, kupitia promotion hii unaweza kujipatia zawadi mbalimbali kama vile King’amuzi, Brenda, headphone speakers na zamadi nyengine nyingi pindi utembeleapo maduka yote ya simu nchini Tanzania yenye promotion.
Baadhi ya maduka yenye promotion yametajwa kwa Dar es Salaam Infinix Smart Hub Mlimani City na Kariakoo, Ram 4, Animol 1, Jumbo na mengineyo kwa Mikoani tunapatikana Arusha Summit Centre, Nena Shop kwa Mwanza ni Tuzo Mobile na Luis shop.
“Promotion hii ya TUPO LIVE itadumu kwa muda wa week mbili ilianza rasmi tarehe 15/10 na tutaitimisha tarehe 30/10/2020. Karibuni sana katika maduka yetu yote ya simu mjipatie Infinix HOT 10 toleo jipya kabisa lenye sifa lukuki kama vile; Processor aina ya MediaTek Helio G70, battery yenye ujazo wa 5200mAh, kamera zenye megapixel 16+2+2+QVGA kwa megapixel 8 selfie, memory yenye GB 64+GB 3RAM, kioo cha nchi 6.78 na teknolojia ya DTS Audio” alisema Aisha Karupa, Afisa wa mahusiano wa kampuni ya Infinix.