Home Mchanganyiko SERIKALI YARIDHISHWA NA MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI NJOMBE

SERIKALI YARIDHISHWA NA MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI NJOMBE

0
……………………………………………………………………..
Wakazi wa kata ya Ninga tarafa ya Lupembe wilayani Njombe wapo mbioni kuanza kunufaika na mradi wa maji unaojengwa katika kijiji cha Ninga wenye thamani ya zaidi ya mil mia 560
Kuanza kutekelezwa kwa mradi huo ambao kwa muda mrefu ulikuwa ukisubiliwa kuwasukuma wananchi kuwa na moyo wa kufanikisha ujenzi kwa wakati kwa kushirikiana na watalaamu kutoa nguvu kazi na vifaa visivyopatikana madukani ili uweze kukamilika kwa wakati na kuanza kunufaisha wananchi.
Fredrick Damian Miale mwenyekiti wa kijiji na Amina Shorongo ni baadhi ya wakazi wa Ninga ambao wanasema kwa kipindi kirefu akina mama wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa zaidi ya km 2 hadi 3 kufata maji mabondeni hali ambayo inawafanya kupoteza muda mwingi na kurudishwa nyuma kiuchumi.
Wamesema endapo mradi huo utakamilika utawafanya kutekeleza kampeni ya nyumba ni choo kwa asilimia 100 na kukabiliana na magonjwa yatokanayo na uchafu kwa kuwa kutakuwa na maji ya kutosha ambayo ni muhimu katika kupambana na uchafu.
Awali akizungumzia mradi huo Fundi Sanifu kutoka wakala ya usambazaji maji  safi na usafi wa mazingira vijijini Ruwasa Joakimu Sanga amesema utatekelezwa kwa kutumia false akaunti ambapo vituo vya maji 29 na mitandao ya maji itajengwa,In take,Nyumba ya mlinzi na Pampu pamoja na Tenki lenye mita 8 lenye ujazo wa mita elfu 1000,
Aidha Sanga amesema mafundi wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho kwani walikuw tayari muda wote kujitokeza kuchimba mitaro,mashimo na kusogeza vifaa vya ujenzi huo ambacho umekuwa na kiu ya muda mrefu kwa wananchi.
” Kukamilika kwa mradu huu kutawafanya wakazi wapatao 2756 kijiji cha Ninga kunufaika na huduma hiyo ambayo muhimu kwa maisha ya binadamu,Alisema Joakim Sanga.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kitengo cha manunuzi kutoka wizara ya maji Dr Christopher Nditi akiwa na timu ya watalaamu kutoka wizarani ameridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi mingi ya maji katika mkoa wa Njombe na kudai serikali imekusudia kumtua ndoo mama kichwani kwa kukamilisha miradi ya maji katika maeneo ya mijini na vijijini.
Dr Nditi ambaye amekagua miradi mbalimbali ya maji ukiwemo wa Howard Kibena, Ninga ,Kitole na Matembwe amesema katika ukaguzi huo wamebaini changamoto kadhaa ikiwemo ya miundombinu ya maji, Mtandao mdogo wa maji katika mradi wa kibena na kuahidi kwenda kuzitafutia majibu haraka iwezekanavyo.
Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 24 ya Tanzania mkurugenzi huyo amesema mchakato upo katika hatua nzuri na Njombe ni miongoni mwa miji iliyofadhiliwa na serikali ya India kutekeleza mradi wa maji 
” Ni kwenye Njombe ni moja na miji 24 ya Tanzania ambayo imeingizwa kwenye mpango wa ujenzi wa miradi ya maji itakayotekelezwa kupitia fedha ya India , na pindi itakapoanza kutekelezwa itachukua muda mrefu kidogo wa kuanzia mwaka mmoja hadi mitatu,Alisema Dkt Christopher Nditi. 
Nae mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na taka mji wa Njombe mhandisi John Mtyauli akielezea changamoto ya huduma ya maji katika mji wa Njombe ,anasema licha ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Howard Kibena lakini bado mji wa Njombe unakumbwa na adha ya maji kwasababu ya kasi ya ongezeko la watu.
Eng Mtyauli amesema mahitaji ya maji ya mji wa Njombe ni makubwa ikilinganishwa na idadi ya watu hivyo wanategemea kuwa endapo mradi mkubwa unaotarajiwa kujengwa katika mto wa Hagafilo utakamilika utamaliza shida ya maji katika mji huo na kuufanya mgao kuwa historia.
“Njombe inakasi kubwa ya Ongezeko la watu kutokana na uchanga wake na fursa zilizopo hivyo kiwango cha maji kinachozalishwa kinashindwa kukidhi mahitaji ya watu,Alisema eng John Mtyauli.
Timu hiyo ya watalaamu kutoka wizara ya maji ikiongozwa na Dr Nditi imetembelea na kukagua mradi wa Howard Njombe mjini,Ninga,Matwembwe na Kitole Ukarawa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Njombe.