*****************************************
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dr Hussein Ali Mwinyi amesema kwa anaimani chama chake kitaibuka mshindi katika uchaguzi wa October 28 kutokana na tathmini ya muitikio wa wananchi katika mikutano ya kampeni nakukutana na makundi maalum kisiwani Pemba.
DR Hussein Ali Mwinyi ambae ni mgombea urais wa Zanzibar ameeleza hayo nje ya ukumbi wa mkutano na mabalozi wa mkoa wa kaskazini Pemba alipokutana nao kuwakumbusha wajibu wao siku ya uchaguzi wa October 28 mwaka huu .
Amesema wingi wa wananchi na wananchama wa CCM waliojitokeza katika mikutano yake ya kampeni ni ishara tosha ya ushindi wakishindo kuanzia ngazi ya Udiwani ,Uwakilishi Ubunge na Urais.
Akizunguymzkia uchumi wa Zanzibar amesema sekta ya viwanda ndio chanzo kikuu cha mapato, kwenye kutekeleza ahadi za maendeleo nakukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Katika mkutano na mabalozi hao amewataka viongozi hao wangazi ya Chini katika chama kuhakikisha wananchi wao wanajitokeza kupiga kura za ushindi kwa CCM.
Mkutano huo wa mgombea urais wa Zazibar kwa tiketi ya CCM, ulilenga kuwakumbusha mabalozi wajibu wao siku ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika October 28.