Home Michezo YANGA YAMTAMBULISHA KAZE KUWA KOCHA MPYA,ASAINI MIAKA MIWILI

YANGA YAMTAMBULISHA KAZE KUWA KOCHA MPYA,ASAINI MIAKA MIWILI

0
………………………………………………………………………………………………………
KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi leo kocha mpya raia wa Burundi Cedric Kaze na kumpa kandarasi ya miaka miwili, Ambapo zoezi la utiaji saini limefanyika katika makao makuu ya klabu hiyo iliopo mitaa ya twiga na Jangwani kariakoo, Jijini Dar es Salaam.
Kaze anachukua mikoba ya Zlatko Krmpotić ambae aliondoshwa klabuni hapo baada ya kushindwa kuleta muunganiko ndani ya kikosi na mchezo wa kuvutia uwanjani.
Kaze hapo awali alikuwa akifundisha academy ya Barcelona nchini Canada, ujio wake katika klabu ya Yanga huwenda tukashudia kandanda la ushindani na kuvutia (Pira kisheti pira makange).
Kocha huyo amewambia mashabiki na wapenzi wa yanga kuwa watafurahia mpira mzuri.
“Siwahakikishii ubingwa kitu ambacho ninawahakikishia mashabiki wa yanga watakuja kwenye mechi watafurahi, Watatoka wanaimba na watasema kesho yake watakuja tena kuangalia yanga.”Amesema Kaze.
Klabu hiyo inakiu ya ubingwa mara baada kukosa ubingwa huo kwa misimu mitatu mfululizo.