Home Mchanganyiko KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI ASAFIRI NA TRENI YA KIHANDISI YA...

KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI ASAFIRI NA TRENI YA KIHANDISI YA YAPI MERKEZI KUKAGUA MRADI WA TRENI YA UMEME (SGR)

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli TRC Bw. Masanja Kadogosa eneo la Soga wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa treni ya Umeme SGR kipande cha Dar- Moro akiongozana na waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali leo Ijumaa Oktoba 16,2020.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-MRADI WA SGR RUVU)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas akipanda kwenye treni ya Kihandisi ya Yapi Merkezi wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa treni ya Umeme SGR kipande cha Dar- Moro akiongozana na waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali leo Ijumaa Oktoba 16,2020.

Ilikuwa ni siku nzuri kwa DJ maarufu wa CCM Dj Sweety Lady wakati akikata keki kusherehekea siku yake ya kuzaliwa katika treni hiyo ya Kihandisi wakati wa ziara hiyo leo kulia ni Msanii Shishi Baby.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Hassan Abbas  na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli TRC Bw. Masanja Kadogosa  wakimpigia makofi Dj Sweety Lady wakati akikata keki kwenye treni hiyo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa treni ya Umeme SGR kipande cha Dar- Moro.

Wasanii mbalimbali wakiwa kwenye treni hiyo wakifurahia safari.

Mwanamuziki Mrisho Mpoto akifungua chupa ya mvinyo kusherehekea siku ya kuzaliwa ya DJ Sweety Lady.

Majadiliano kabla ya kupanda treni Peter Msechi,Monalisa katikati na Shishy Baby.

Mwigizaji wa filamu Natasha akiongozana na wasanii wenzake pamoja na baadhi ya wanahabari kwenda kupanda treni ya Kihandisi ya Yapi Merkezi ili kuendelea na ziara leo.

Msanii wa muziki wa Singeli Snura Mushi ni miongoni mwa wasanii waliojitokeza kuutembelea mradi wa SGR hapa akiongozana na wenzake kwenye kupanda treni ya kihandisi ya Yapi Merkezi tayari kwa safari.

Msanii Sholo Mwamba katikati akiwa pamoja na wenzake katika terni hiyo.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Rodney  akiongozana na wasanii Peter ziara Msechu na Mrisho Mpoto pamoja na baadhi ya maafisa wa Chama cha Mapinduzi CCM kwenda kupanda treni ya Kihandisi ya Yapi Merkezi ili kuanza hiyo.

Treni ya Kihandisi ya Yapi Merkezi ikiwa tayari kuwachukua wasanii pamoja na waandishi wa habari kwa ajili ya kwenda kutembelea mradi wa reli ya umeme SGR.

Baadhi ya wasanii na waandishi wa habari waksubiri kupanda treni ya kihandisi ya Yapi Merkezi kwa ajili ya kuanza ziara hiyo.

 Msanii Shishy  Baby pamoja na baadhi ya maafisa wa chama cha mapinduzi CCM na waandishi wa habari wakipanda kwenye treni ya Kihandisi ya Yapi Merkezi tayari kwa ziara hiyo.