Home Mchanganyiko MUROTO: HAKUNA MHALIFU ATAKAYEBAKI  SALAMA 

MUROTO: HAKUNA MHALIFU ATAKAYEBAKI  SALAMA 

0

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto – SACP akiwaonesha baadhi ya nyara za serikali zilizo kamatwa na jeshi hilo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mkoani Dodoma 

Muonekano wa nyara za serikali na silaha za moto zilizokamatwa na jeshi la Polisi Mkoa wa DodomaBaadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma wakiwa wanaondosha silaha na nyara za serikali zilizokamatwa mezani baada ya kikao cha waandishi wa habari leo mkoani Dodoma.

……………………………………………………………….

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na vikosi vya kupambana na jangili wamefanyikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa nane wa makosa ya kupatikana na silaha pamoja na nyara za Serikali kinyume na sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto – SACP wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mkoani Dodoma 

Muroto amesema kuwa mnamo tarehe 11 Octoba 2020 majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Ikengwa, kata ya Kinyasi , tarafa ya Pahi wilaya ya Kondoa alikamatwa Simoni Nzara (21) akiwa na meno ya tembo mawili ambayo ni nyara za serikali kinyume na sheria .

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pia msako mkali unaendelea dhidi ya watuhumiwa wangine”, ameeleza Muroto

Aidha katika kijiji cha Chaludewa wilayani Mpwapwa wamekamatwa watuhumiwa watatu wakiwa na meno ya tembo vipande viwili ambayo ni nyara za serikali , kinyume na sheria.

Muroto amesema kuwa watuhumiwa hao ni Ganja Masonga (75) mkazi wa Chaldewa- Mpwapwa, Kitereja Nkubha (38) mkazi wa Chiboli – Mpwapwa na Ndalu Nhimko (48) mkazi wa Minjenja – Gairo.

Tukio lingine limetokea katika kata ya Sejeli wilaya ya Kongwa lililohusisha watuhumiwa watatu wakiwa na silaha ya kivita aina ya AK47 yenye namba. UR2716 ikiwa na risasi zake 27 kwenye magazine ambayo wanaitumia katika uharifu wa ujangili.

Watuhumiwa hao ni Juma Mngoya(40) mkulima, John Mohamed(34) mkulima na Jackson Masaka (20) mkulima wote wakiwa wakazi wa Banyibanyi wilaya ya Kongwa.

Muroto ameongeza kuwa huko mtaa wa Kisasa Medelii, Kata ya Makulu amekamatwa Deogratias Masawe(40) fundi ujenzi aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la kumjeruhi kwa risasi binti ambaye  jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama.

Vile vile Muroto ameeleza kuwa sababu ya kutaka kumjeruhi ni gomvi wa kimapenzi na majeruhi amelazwa ICU katika hospitali ya Rufaa ya Dodoma anaendelea na matibabu.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na silaha Bastola aina ya BROWNING CALB 7.65 MAKER Namba A748082,CAR .95632 ikiwa na risasi saba kinyume na sheria na kuitumia katika uhalifu wa kutaka kuhatarisha maisha ya watu wengine.

Uchunguzi zaidi unaendelea il;I kubaini silaha hiyo ameipataje na atafikishwa mahakamani mara upelelezi ikikamilika.