*************************************
NJOMBE
Wakazi kutoka vijiji 5 na vitongoji 21 vya kata ya Mtwango yenye wakazi zaidi ya elfu 14,000 wilayani Njombe wamejitokeza kusogeza mawe na kuchimba msingi katika ujenzi wa majengo 10 ya kituo cha afya katika kata hiyo iliyokuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya matibabu.
Wakizungumzia adha ya matibabu katika kata hiyo wakazi hio akiwemo Mariseli Ndonyalo, Aldo Shaban na Valentino Mwelange wanasema wamekuwa wakilazimika kusafiri umbali wa zaidi ya km 20 kufata huduma za afya katika hospitali ya mji wa Njombe Kibana ama Ikelu jambo ambalo limekuwa likisababisha akina mama kuzidiwa wakiwa njiani .
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Ally Jumah bila hiyana nao wameungana na wananchi kwa kushika sururu na majembe ili kuchimba msingi wa majengo ambayo yatajengwa kwa kutumia false akaunti katika kipindi cha miezi 6
Deusdedit Kalaso ambaye ni mganga mkuu wa halmasahuri ya wilaya ya Njombe kitajengwa kwa awamu mbili huku gharama yake ikiwa ni mil 600
Awali kabla ya kuanza zoezi la ujenzi wananchi hao wakaomba nguvu ya mungu kusimamia mradi huo , zoezi ambalo linaongozwa na mchungaji Mchungaji Osias Mkanyula ambaye kupitia sara ambapo anamuomba mungu kubariki mikono yao.