Home Siasa MSIBA MZITO! SHIGONGO ASIMAMISHA KAMPENI BUCHOSA…

MSIBA MZITO! SHIGONGO ASIMAMISHA KAMPENI BUCHOSA…

0

**********************************

KAMPENI za mgombea wa kiti cha ubunge Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo Jamese zimelazimika kusimama kwa siku moja kupisha shughuli za mazishi ya mmoja wa wapiga kura wake, mzee Tenesi Magina ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana Jumapili, Oktoba 11, 2020 katika Kijiji cha Nyehunge.

Licha ya mzee Magina kuwa ni mpiga kura wa Shigongo, alikuwa pia ni baba mzazi wa Marco Magina ‘Zagallo‘ ambaye ni mfanyakazi wa Makampuni ya Global Group yanayomilikiwa Shigongo.

Oktoba 12, 2020, Shigongo alitarajiwa kufanya kampeni zake kwenye visiwa vya Kome vilivyopo ndani ya jimbo hilo.

Kisiwa hicho kwa sasa ni tarafa ambapo Shigongo alitakiwa kufanya kampeni hizo kwa siku tatu mfululizo, katika kata ya Nyakasasa, Bugata, Buhama na Bugolo, lakini alilazimika kuzikatisha ili aweze kushiriki maziko ya mzee Magina. Shigongo ataaendelea ka kampeni visiwani humo keshokutwa Oktoba 14, mwaka huu.