Kivuko cha MV.UKARA II hapa kazi tu kikielea kwenye maji mara baada ya kushushwa katika Ziwa Viktoria baada ya ujenzi wake kukamilika. Kivuko hicho kilichogharimu shilingi bilioni 4.2 kimejengwa na kampuni yaSongoro, kitafanyiwa majaribio ikiwemo hali ya usalama kabla ya kupelekwa Bugorola Ukara kuanza kutoa huduma na kina uwezo wa kubeba abiria 300 na magari 10 sawa na tani 100.Kivuko cha MV.UKARA II hapa kazi tu kikiwa kimepaki katika yadi ya Songoro wakati kikisubiri kushushwa majini katika Ziwa Viktoria baada ya ujenzi wake kukamilika. Kivuko hicho kilichogharimu shilingi bilioni 4.2 kimejengwa na kampuni ya Songoro, kitafanyiwa majaribio ikiwemo hali ya usalama kabla ya kupelekwa Bugorola Ukara kuanza kutoa huduma na kina uwezo wa kubeba abiria 300 na magari 10 sawa na tani 100.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga wa tatu kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi Mhandisi Lazaro Vazuri Pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa ulinzi na usalama wa mkoa wa Mwanza wakishuhudi zoezi la uteremshaji wa kivuko kipya cha MV.UKARA II Hapa kazi tu (hakipo pichani) lililofanyika katika yadi ya Songoro Ilemela Mwanza.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Major Songoro akiwaeleza viongozi mbalimbali waliofika katika tukio la kuteremshwa kwenye maji kwa kivuko cha MV.UKARA II Hapa kazi tu sifa mbalimbali za kivuko hicho wakati wakisubiri zoezi hilo kuanza. Tukio hilo limefanyika katika yadi ya Songoro iliyoko Ilemela mkoa wa Mwanza.