Home Mchanganyiko UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA WAKUMBWA NA CHANGAMOTO YA MAJI, NAIBU...

UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA WAKUMBWA NA CHANGAMOTO YA MAJI, NAIBU KATIBU MKUU  WIZARA YA MAJI ATOA MAAGIZO.

0

Naibu katibu mkuu wizara ya  Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba kushoto akitoa maelekezo kwa wataalamu wa RUWASA baada ya kufika katika chuo cha ufundi VETA kinachojengwa halmashauri ya wilaya Bukoba Mkoani Kagera kwa ufadhili wa nchi ya China.

Meneja wa RUWASA Kagera Mhandisi Walioba Sanya kulia akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji wanayoisimamia kwa naibu katibu mkuu  wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba kushoto.

Naibu katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akikagua ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita elfu hamsini (50,000) linalojengwa kata nyakibimbiri Halmashauri ya wilaya Bukoba.

Tenki la maji lenye ujazo wa lita laki 5 lililojengwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira BUWASA kwaajili ya kumaliza tatizo la maji kwa kata za Nshambya, Kibeta, Kagondo, Kahororo na Nyanga Manispaa ya Bukoba.

*************************************

Na Allawi Kaboyo- Bukoba.

Mradi wa ujenzi wa chuo cha VETA Kagera unaotekelezwa na serikali ya China umeshindwa kukamilika kwa wakati uliopangwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya Maji.

Taarifa hiyo imetolewa na mhandisi Franck Thomas ambaye ni msimamizi wa ujenzi na mwakilishi wa serikali ya Tanzania mbele ya Naibu Katibu mkuu wizara ya Maji alipofanya ziara katika mradi huo kuangalia uwezekano wa kufikisha huduma ya Maji Okitoba 12, Mwaka huu.

Thomas ameeleza kuwa mradi huo ulitakiwa kukamilika mwaka huu lakini kutokana na changamoto za Corona pamoja na kutokuwepo kwa huduma ya Maji vimesababisha mradi kuzorota kwa kuwa Maji wanayoyatumia pale wanalazimika kuyasomba kwa magari kutoka kwenye vimito vidogo vodogo.

Amesema kuwa Mahitaji kwa siku ni Lita elfu 50 hali ambayo inawapelekea kutumia gharama kubwa ya kusomba Maji na wakati mwingine kusababisha kusimama kwa kazi mbalbali kwa kutumia muda mwingi kusubiri Maji.

Akijibu hoja hizo Naibu katibu mkuu wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuongeza kuwa wizara inalitambua hilo na ndio maana amefika ili kuona namna ya kulimaliza tatizo hilo.

Ameelekeza watendaji wa wakala wa Maji RUWASA kuanza utekelezaji wa mradi huo wa Maji mapema mwezi Novemba na wahakikishe ifikapo mwezi machi mwakani Maji yawe yamefika Chuoni hapo na kuanza kutumika.

Ameongeza kuwa mtandao huo ambao uawanufaisha na wananchi wa kijiji Burugo ambapo mtandao mzima urefu wake ni km12.

Awali akiongea na watumishi wa BUWASA pamoja na RUWASA amewataka watumishi hao kutokaa maofisini na badala yake waitembelee miradi ili kuweza kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi ili kupunguza malalamiko kwa wananchi.

Aidha Mhandisi Nadhifa akikagua tanki la Maji lenye ujazo wa Lita laki 5, ameipongeza BUWASA kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maji katika miradi mbalimbali wanayopewa kusimamia.

Naibu katibu mkuu wizara ya Maji ameendelea na ziara yake mkoani Kagera yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya Maji katika halmashauri za Manispaa ya Bukoba, Halmashauri ya wilaya Bukoba na Halmashauri ya wilaya Muleba.