Mkuu Wilaya ya Morogoro Mhe Bakari Msulwa akizungumza kwenye kongamano lililoandaliwa na Chuo kikuu huria kituo cha Morogoro katika kuelekea siku ya mtoto wa kike dunia.
Kaimu Makamu Mkuu wa chuo teknolojia za kujifunzia huduma za Mikoani Dr Hariet Hellar akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Chuo kikuu huria kituo cha Morogoro katika kuelekea siku ya mtoto wa kike dunia, ambapo amewataka wadau kutumia siku ya mtoto wa kike duniani kuwafika mabinti walio katika mazingira magumu.
Baadhi ya wadau aliojitokeza kwenye kongamano Hilo.
Picha ya pamoja
……………………………….
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO.
Jamii na Wazazi Nchini wamekumbushwa kuendelea kumlinda mtoto wa kike na vitendo vya unyanyasaji vinavyomkandamiza haki zake za msingi ambavyo mala nyingi vimekuwa vikitendwa na ndugu wa karibu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Bakari Msulwa wakati akifungua kongamano lililoandaliwa na Chuo kikuu huria kituo cha Morogoro katika kuelekea siku ya mtoto wa kike dunia kwa lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali na kujadili mambo yanayomuhusu mtoto wa kike.
Akizungumza katika kongamano hilo Mhe Msulwa alisema kuwa jukumu la kumlea watoto wa kike sio la mzazi pekeake bali ni jukumu la jamii pamoja na mtoto mwenyewe,katika kukizingatia na kuwa na nidhamu kwa yale yote anayofundishwa na watu walimzidi umri.
Kwa upande wake,Kaimu Makamu Mkuu wa chuo teknolojia za kujifunzia huduma za Mikoani Dr Hariet Hellar amesema wao kama chuo wameona ni muhimu kuwakutanisha wadau ili waweze kujadili mambo mbalimbali yanayomuhusu mtoto wa kike,hususani katika kipindi hiki ambacho dunia inadhimisha siku ya mtoto wa kike.
Aidha amewataka wadau kutumia maadhimisho hayo kuwa kama fulsa ya kuweza kuwatembelea watoto wa keki walio katika mazingira magumu pamoja na kuafanya mambo mbalimbali yatakayoweza kumjenga mtoto wa kike ambaye ni mama wa badaye katika msingi mzuri.
Nae Mkurugenzi wa chuo kikuu huria kituo cha Morogoro Dr Wambula Rangi amewataka watoto wa kike kuwa na nidhamu kwa walezi wao ili kuweza kutimizia ndoto zao na kuondokana na hali ya ukatili dhidi yao hasa kwa kukosa haki za msingi.
Nao baadhi ya watoto wa kike waliohudhuria kongamano hilo wakitoa shuhuda, wamekili kukutana na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia na kutokupewa kipaumbele na heshima katika jamii,huku wakiwataka wazazi kuwa makini na marafiki wa watoto wao bila ya kujali jinsia.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Jeshi la Porisi kitengo cha dawati la jinsia,Madkatari na washauri kutoka taasisi mbalimbali za vyuo vikuu.