*************************************
Ikiwa zimebaki siku 16 kusikia kipyenga cha fainali ya uchaguzi mkuu wa October 28, 2020 nchini Tanzania, leo October 12, 2020 nakusogeza karibu na mkutano wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dr. Tulia Ackson akiwa katika kata ya Iyela ambapo alikuwa akiwaeleza ni kwanini Wananchi hao wakipigie kura zote za ndio chama chake itakapofika siku ya kupiga kura.
“Safari hii Mbeya Mjini tunataka hoja za maendeleo na tunaenda na Tulia anayetulia Bungeni, leo nitawaeleza ni kwanini ukiamini Chama Cha Mapinduzi, kwanini Umuamini John Magufuli, Kwanini Umuamini Tulia Ackson na kwanini uwaamini Madiwani wanaotokana na CCM”
“Nikiachana na mambo mengi yaliyobainishwa katika Ilani ya CCM kwa mwaka 2020-2025 yaliyobainishwa kufanyika chini ya Rais Magufuli wacha kwanza niwape machache tu ambayo mimi Mbunge wenu nimekwishayafanya hata kabla ya kuja kwenu kuwaomba kura. Na hapa nitawaeleza machache tu kwenye Kata hii ya Iyela na wala hatukimbilii mbali kwanza”
“Hapa Iyela shule zetu za msingi Nero na Mapambano walikuwa na changamoto ya choo na kazi imeanza, shule ya msingi Pambogo na Airport wanachangamoto za miundombinu walinieleza na tunapozungumza tayari nilishapeleka mifuko 200 ya Cement, sasa hiyo ni mifano michache tu hapa mkiwa hata mlikuwa hamjatupa nafasi sasa mkitupatia tutawafanyia makubwa zaidi”
“Niende kwenye elimu ya Sekondari, tunayo shule yetu ya Sekondari Iyela pamoja na Samora mimi Mbunge wa kujiongeza Shule ya Sekondari Iyela tumepeleka pale mifuko 358 ya Cement ambayo ni zaidi ya million sita tumeweka pale kwasababu walikuwa na uhaba wa madarasa sisi tukashusha mzigo pale, tumepeleka mabati 100 zaidi ya Milion mbili na laki saba. Sasa ndugu yangu mtu akija kwako kukuomba kura muulize umetufanyia nini kabla? Huu ni muda wa hesabu na kama mtu hakufanya kazi tunasukuma nje”
“Shule ya Sekondari Samora pale tumepeleka computer tano na printers ambazo ni Tsh: 10,750,000/-, sasa wapo watu wanapita huko pamoja na mfuko wa Jimbo tuwaulize umefanya nini kwetu Iyela? Na anapaswa awe ametufanyia makubwa zaidi ya ambayo Tulia ametufanyia bila mfuko wa Jimbo.”