…………………………………………………………………………………………………
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU 12 KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAKOSA MBALIMBALI YA KIUHALIFU.
TAREHE 06.10.2020 MAJIRA YA 11:00HRS HUKO KATIKA MAENEO YA MJINI KATI, WILAYA YA NYAMAGANA, MKOA WA MWANZA, JESHI LA POLISI LILIWAKAMATA WATU WA NNE AMBAO NI 1.YELEMI BADRU ATHUMAN, MIAKA 45, MHAYA, DEREVA, MKAZI WA TUANGOMA – DAR ES SALAAM, 2.MUSSA JUMA MUSSA, MIAK 44, MHAYA, MFANYA BIASHARA WA MATOFALI, MKAZI WA NSHAMBA –MULEBA, 3.RUTAYISIRE PATRICK MANDE, MIAKA 38, MKULIMA, RAIA WA UGANDA, MAKAZI YAKE MTUKULA NA 4. DELPHINA ANTHONY KUNGU, MIAKA 51, MNYATURU, MKULIMA, MKAZI WA ILONGERO –SINGIDA, KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAKOSA YA UTAPELI JIJINI MWANZA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA WAKIWA NA DOLLAR ZA KIMAREKANI 192, KATIKA MCHANGANUO WA NOTI MOJA YA DOLLA 100 NA NOTI 92 ZA DOLLA MOJA SAWA NA FEDHA ZA KITANZANIA TSHS 441,000/=. VILEVILE WALIKAMATWA WAKIWA NA FEDHA ZA KITANZANIA KIASI CHA TSHS127, 000/=, MAKARATASI YALIYOKATWA MITHILI YA NOTI YALIYOFUNGWA KWA PAMOJA NA KUWEKWA KWENYE BAHASHA. PIA WALIKAMATWA WAKIWA NA GARI NAMBA T.205 BGW AINA YA CHASSER RANGI NYEUPE AMBAYO WANAITUMIA KATIKA KUTENDA UHALIFU MAENEO MBALIMBAILI.
AIDHA BAADA YA KUHOJIWA KWA KINA WATUHUMIWA HAO WAMEKIRI KUJIHUSISHA NA MATUKIO YA UTAPELI KATIKA MIKOA MBALIMBALI YA NCHI YETU IKIWEMO DAR ES SALAAM, MBEYA, ARUSHA, TANGA, KIGOMA NA BAADHI YA NCHI JIRANI AMBAZO NI
PAMOJA NA UGANDA, ZAMBIA NA KENYA. HATA HIVYO MATAPELI HAO WAMEELEZA MBINU WANAYOTUMIA KUTAPELI KUWA WANAKWENDA NDANI YA BANK NA KUJIFANYA HAWANA UELEWA WA TARATIBU ZA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI AMBAPO HUTAJA KIWANGO CHA CHINI CHA UBADILISHAJI WA DOLLA ZA KIMAREKANI NA KUOMBA MSAADA KWA MTEJA WALIOMLENGA BAADA YA KUBAINI KUWA ANA FEDHA NYINGI ILI AWASAIDIE KUJAZIWA FOMU NA BAADAE MTEJA HUYO AKIKUBALI NA KUINGIA TAMAA YA KUPATA FAIDA KIRAHISI WANAMRUBUNI NA KUTOKANAE NJE YA BANK NA KWENDA SEHEMU NYINGENE AMBAZO MARA NYINGI NI MAENEO YA HOTEL AMBAPO UTAPELI HUO HUFANYIKA KWA KUJIPATIA FEDHA HALALI ZA KITANZANIA ZENYE THAMANI KUBWA NA WAO KUMPA ANAYETAPELIWA BAHASHA YENYE MAKARATASI NA WAKATI MWINGINE BAHASHA YENYE DOLLA ZA KIMAREKANI YENYE THAMANI NDOGO. UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAKAMILISHWA NA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA MOJA.
TUKIO LA PILI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LILIWAKAMATA WATU 8 KWA TUHUMA ZA KUCHANA MABANGO YA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UBUNGE NA UDIWANI WA CHAMA CHA CHADEMA NA CCM KATIKA MAENEO TOFAUTI YA WILAYA YA NYAMAGANA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA. AIDHA KATI YAO WATUHUMIWA WATANO WALIFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUTIWA HATIANI AMBAPO WALIHUKUMIWA VIFUNGO KUANZIA MIEZI MITATU HADI MINNE. WATUHUMIWA HAO NI:-
- MASALU BULULI, MIAKA 24, MSUKUMA, KONDA WA DALADALA, MKAZI WA IGOMA.
- STEVEN AUGUSTINO, MIAKA 22, MSUKUMA, MJASILIAMALI, MKAZI WA IGOMA.
- JOHN JUMA, MIAKA 20, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA IGOMA
- AMANI STEPHANO, MIAKA 33, MUANGAZA, MKULIMA, MKAZI WA BUGARIKA.
- ABUU ABUBAKARY, MIAKA 28, MFANYABIASHARA, MKAZI WA KANYERERE MAINA.
WATUHUMIWA WAWILI AMBAO NI; i. SAMWEL MATONGO, MIAKA 32, MJASILIAMALI, MKAZI WA BUGARIKA, ii. SELEMAN ISSA, MIAKA 25, MKULIMA, MKAZI WA BUTIMBA, KESI ZAO ZIMEFIKISHWA MAHAKAMI NA MTUHUMIWA MMOJA AMBAYE NI ABBAS GERAD, MIAKA 33, MUHA, MKULIMA NA MKAZI WA
MALIMBE, UPELELEZI DHIDI YA TUHUMA ZINAZOMKABILI UNAENDELEA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA BAADHI YA WANACHI WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA KIUHALIFU WAACHE KWANI IKIBAINIKA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA MARA MOJA. AIDHA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUWASHUKURU WANANCHI KWA KUTOA USHIRIKIANO KWA KUTUPATIA TAARIFA ZA WAHALIFU NA UHALIFU KWA WAKATI.
IMETOLEWA NA;
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
09 OCTOBER, 2020