Home Mchanganyiko SHIRIKA LA POSTA DODOMA LAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUBORESHA...

SHIRIKA LA POSTA DODOMA LAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUBORESHA HUDUMA ZAO

0

Afisa Mwandamizi Mkuu wa Shirika la Posta Dodoma,Michael Mwanachuo,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Mfanyakazi wa Shirika la Posta Dodoma,akiwalisha keki wateja wake waliofika ofisini hapo kujumuika na watumishi wa shirika hilo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

SHIRIKA la Posta Tanzania Mkoa wa Dodoma limeadhimisha  wiki ya huduma kwa wateja kwa kukata keki pamoja na wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Afisa Mwandamizi Mkuu wa Posta Dodoma, Michael Mwanachuo,amesema kuwa wamejipanga kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa kuanzisha smart postal ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Mwanachuo amesema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja tumekuja kutoa  msaada wa vyakula na vinywaji kwenye Kituo cha kulea watoto wenye utindio wa ubongo cha Miyuji Cheshire.

“ Tumeguswa na mahitaji ya watoto hasa wenye mahitaji maalum ndio maana katika kuadhimisha Siku ya Posta Duniani tumeamua tuje kuwaona watoto na kutoa zawadi”amesema Mwanachuo

Mwanachuo amesema kuwa katika kuboresha huduma kwa wateja   shirika hilo limeamua kuleta  huduma mpya ya wananchi kumiliki sanduku la barua kwa kutumia namba ya simu.

“Tumeamua kuboresha huduma kwa wateja wetu kwa kuwa na sanduku la barua kwa simu yake ya mkononi, haitaji kuwa na sanduku kama ilivyokuwa awali”amesema Mwanachuo.

Mwanachuo amesema kuwa Mtu akiwa na Smart postal (sanduku kiganjani mwako), itamuondolea hata ile adha ya kufunga safari kuja kufungua sanduku lake na wakati mwingine unakuta  halina barua.

Mwanachuo amesema kuwa  azma ya Shirika ya kuhakikisha inatoa huduma kwa haraka za usambazaji na utumaji barua, nyaraka, vifurushi na vipeto katika kata na vijiji vya Mkoa wa Dodoma.