DAR ES SALAAM
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema hadi sasa wananchi wengi wamekuwa watulivu licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu wachache walioandaliwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kufanya vurugu na kujiingiza kwenye uhalifu.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kuwataka baadhi ya viongozi kufanya masuala ya siasa na kuacha kuwatumia vijana na kuwaingiza kwenye uhalifu na kwamba yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
Kuhusu upigaji wa kura Zanzibar, IGP Sirro amesema, wapo baadhi ya watu wanaohamasisha baadhi ya watu au kikundi cha watu kuvunja sheria wakati wa zoezi la upigaji kura kinyume cha sheria, kanuni na taratibu zilizopo.