**********************************
Na Farida Saidy,Morogoro.
Wasaidizi wa watunga Sera wa Ofisi ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na wale wa Ofisi ya Waziri Mkuu wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili sera zinazotungwa Bungeni ziwe zinye kuakisi matakwa ya watanzania.
Akizungumza mjini Morogoro wakati wa warsha iliyo wakutanisha wasaidizi watunga Sera pamoja na baadhi ya maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kujengewa uwezo juu ya masuala mtambuka ya utungaji wa Sera, ambapo Katibu wa Bunge Steven Kagaigai amewataka watumishi hao kuzingatia utatuzi wa changamoto za wananchi.
“Ni vyema sasa kila mmoja wenu azingatie weledi wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake ili kuhakikisha kazi ya utungaji wa Sera iwe rahisi na yenye kuendana na matakwa na matarajio ya wananchi”Alisema Steven Kagaigai-Katibuwa Bunge.
Aidha Steven amesema kuwa mipango, Sera na Sheria zinazotungwa huzingatia maslahi ya Wananchi kwani Tanzania ni nchi yenye Serikali inayowekwa na Wananchi, hivyo inaangalia zaidi maslahi ya Wananchi, kwa hiyo Sera isiyozingatia uhalisia wa changamoto zinazowakabili Wananchi itapelekea kutungwa Sera na Sheria zisizofaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi inayo jishughulisha na utafiti wa masuala ya uchumi na maendeleo. (REPOA) Dokta Donald Mmari, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwaandaa watumishi hao kabla ya bunge la 12 halijaanza ili kuwawezesha kufanya kazi wazingatie utaratibu uliopo.
“REPOA tuna ushirikiano mkubwa na ofisi ya Bunge kwa hiyo tukaona umuhimu wa kuwajengea uwezo ili wakati Bunge la 12 litakapoanza wawe na uwezo wa kukabiliana na kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yao” alisema Dokta Mmari.
Hata hivyo Dokta Mmari amesema endapo watumishi hao watakuwa na uelewa mmpana wa kutumia tafiti itwawasaidia kutimiza malengo ya Taifa ya kuwaletea Wananchi maendeleo.