Home Mchanganyiko RAIS MHE.DKT.JOHN MAGUFULI AMETENGUA MAAMUZI YALIYOTANGAZWA NA MHE.SAMAKAFU KUHUSU KUFUTWA KWA MITAALA...

RAIS MHE.DKT.JOHN MAGUFULI AMETENGUA MAAMUZI YALIYOTANGAZWA NA MHE.SAMAKAFU KUHUSU KUFUTWA KWA MITAALA YA ELIMU KWA NGAZI YA CHETI

0

**************************************

RAIS John Magufuli ametengua Maamuzi yaliyotangazwa na Naibu Katibu Mkuu Ave Maria Semakafu kuhusu kufutwa kwa mitaala ya Elimu kwa ngazi ya cheti.

Uamuzi wa Rais Magufuli umekuja saa chache baada ya Semakafu kutangaza mtaala mpya wa ualimu utaanzia ngazi ya Diploma, hata hivyo alisema kwa walimu waliopo mashuleni wataendelea na kazi na kupata muda wa kujiendelea kama watapenda.

Hata hivyo Rais Magufuli amepiga simu kwenye Kongamano la Walimu linaloendelea Mjini Dodoma ikiwa leo ni siku ya walimu amesema ” Kuna tangazo linazunguka kuhusu kufutwa kwa mtaala ngazi ya cheti, lipuuzeeni, limetolewa na watu wabaya, tulianza na nyinyi tutamaliza na nyinyi.

” Mke wangu ni mwalimu ngazi ya cheti, mke wa Waziri Mkuu Majaliwa ni mwalimu ngazi ya cheti, tunawathamini, ndio maana tumetoa nafasi za ajira 13,000,” amesema Magufuli