MGOMBEA Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wake wa kampenin
uliofanyika katuika Uwanja wa Mnazi mmoja Jijini Zanzibar na kuwaombea
kura Wananchi wa Zanzibar na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar
Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi pamoja na Wabunge, Wawakilishi na
Madiwani wa CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe Ali Hassan Mwinyi
akisalimiana na Mgombea Urais wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM
Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzxania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar
kuhudhuria Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania uliofanyika
leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)
MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
MheDkt. John Pombe Magufuli akisakata rumba na Msanii wa muziki wa
Kizazi kipya Zuchu wakati alipopanda jukwaa la wasanii katika uwanja wa
Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar wakati wa mktano wake wa kampeni uliofanyika
leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu) MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Mhe, Dkt.
John Magufuli akilisakata rumba wakati wa mkutano wake wa kampeni
uliofanyika uwanja wa Mnazi Mmoja leo 3/10/2020 na (kushoto kwake)
Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Hussein Mwinyi na Makamu Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine wa CCM
wakijumuika katika kulishata rumba na msani Zuchu.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa Mgombea
Urais wa Tanzania Mhe. John Magufuli uliofanyika Uwanja wa Mnazi Mmoja
Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WANACHAMA wa Cha Cha Mapinduzi Zanzibar wakishangilia
wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Magufuli (hayupo pichani) akihutubia na kuwaombea Kura Mgombea Urais wa
Zanzibar Mhe Dk. Hussein Mwinyi na Wabunge, Wawakilishi na Madiwa wa
CCM, wakati wa mkutano huo uliofanyika uwanja wa mnazi mmoja Jijini
Zanzibar leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwapungia mkono Wananchi wa Zanzibar alipokuwa
akiwasili katika uwanja wa mnazi mmoja kuhudhuria mkutano wa kampeni wa
CCM wa Mgombea Urais wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli leo
3/10/2020.(Picha na Ikulu)
MGOMBEA Urais wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa CCMTaifa
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia WanaCCM na Wananchi
waliohudhuria mkutano wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa mpira
Mnazi Mmoja leo 3/10/2020, na Kushoto kwake) Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Dkt. Bashiru Ally, wakielekea katika jukwaa kuu la Viongozi.(Picha na
Ikulu) VIONGOZI wa Jukwaa Kuu wakiwa wamesimama wakati wakiitikia dua
ikisomwa na Sheikh Sharif Abdulraham Muhidin (hayupo pichani) kabla ya
kuaza kwa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Mpira
Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakishangilia
wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya
CCM Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi
Mmoja leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae
pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa
Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli
uliofanyika katika Uwanja Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo
3/10/2020.(Picha na Ikulu)
WAKE wa Viongozi wakifuatilia hutuba ya Mgombea Urais wa
Tanzania Mhe.John Pombe Magufulia akiwahutubia Wanachama wa CCM Zanzibar
katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja
Jijini Zanzibar leo 3/10/2020 na kuwaombea Kura Mgombea Urais wa
Zanzibar Mhe. Hussein Mwinyi na Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM
na kujiombea kura yeye mwenyewe kwa Wananchi.(Picha na Ikulu)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akihutubia wakati
wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar na
kuwaomba kura Wananchi wa Zanzibar na kumuombea Kura Mgombea Urais wa
Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli na Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani
wa CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)
*************************************