…………………………………………………………………………………….
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM Dr. Tulia Ackson ameshiriki kampeni zake katika kata ya Nsoho jijini humo kwa lengo la kuwaomba Wananchi kumpa ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi hiyo ya Ubunge pamoja na kuwanadi viongozi wengine kupitia chama chake wakiwemo Madiwani pamoja na Rais.
Akiongea na Wananchi hao Dr. Tulia amesema>>>”Ndugu zangu wana-Nsoho mimi huwa nasema wazi kwamba huu ni muda wa hesabu, mtu anapokuja kwenu kuomba kura kwanza muulizeni amewafanyia nini? Kama mtu hajawafanyia lolote Sukuma nje.. safari hii yule tuliyekata naye kuni ndio wa kuota naye moto. Wana-Nsoho sisi CCM tunapokuja hapa tumeshafanya mengi na kupitia irani hii tutawafanyia mengi zaidi”-Dr. Tulia Ackson
“Najua utakuwa umeshasikia mahali kwamba mimi naitwa Mbunge wa kujiongeza, Shule yetu ya msingi Nsoho tulifika tukakuta changamoto mbalimbali ikiwemo za miundombinu na tukapeleka pale mifuko 100 ya cement na hiyo sio kutoka kwenye mfuko wa Jimbo bali ni mfuko wa Dr. Tulia Ackson, Twende shule ya sekondari Nsoho pale nilisimamishwa na wanafunzi wakaniambia wanahitaji Computer na printer sasa nipeni kura Mama wa connection nikawafanyie kazi”-Dr. Tulia Ackson
“Ndugu zangu msiwe na wasiwasi, hizi changamoto tulizonazo hapa ikiwemo elimu, afya, miundombinu na mengineyo ambayo hata mimi mwenyewe nimezishuhudia ikiwemo ubovu wa barabara basi mfahamu wazi kwamba safari hii tunataka tuzimalize hizi. Kwa kukuhakikishia tu ni kwamba haya sio maneno tu tayari kila kitu kipo kwenye hii ilani yetu ya CCM iliyojitosheleza”-Dr. Tulia Ackson