Home Michezo YANGA YAPELEKA SALAMU MSIMBAZI, BAADA YA KUINYUKA COASTAL UNIONI MABAO 3-0

YANGA YAPELEKA SALAMU MSIMBAZI, BAADA YA KUINYUKA COASTAL UNIONI MABAO 3-0

0

*******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Yanga inaendelea kujiweka vizuri baada ya kufanikiwa kuinyuka Coastal Union ya Tanga mabao 3-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam hii leo.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake kwani mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafunguna japo Yanga ilionekana kuwa na huitaji wa kupata mabao kwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Yanga ilizidi kuwa wa moto hasa baada ya kuwapumzisha wachezaji wao kadhaa na kuwaingia wachezaji ambao waliweza kuonesha hali nzuri na kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi kwa mabao 3-0.

Dakika ya 48 ya mchezo Yanga ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa kiungo Mshambuliaji kutokea Ureno Carlinho ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa akipokea krosi upande wa kulia kupitia kwa Deusi Kaseke.

Hata hivyo baada ya dakika nne mbele Yanga ilipata bao la pili kupitia kwa Kiungo wao raia wa Rwanda Haruna Niyonzima mnamo dakika 52 ya mchezo.

Yakouba Songne alifunga mahesabu kwa kupachika bao la tatu dakika 64 na kuisaidia klabu hiyo kuondoka na ushindi wa magoli mengi.