Home Mchanganyiko UN YAMUUNGA MKONO RAIS DKT MAGUFULI KUTOKOMEZA UKATILI WA MWANAMKE IKUNGI

UN YAMUUNGA MKONO RAIS DKT MAGUFULI KUTOKOMEZA UKATILI WA MWANAMKE IKUNGI

0

 

Mkuu wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza baada ya uzinduzi wa mradi kushoto ni  Mwakilishi Mkazi wa
Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan
Milisic

Picha
ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na
wawakilishi wa mashrika ya umoja wa mataifa ,wadau wa maendeleo na kmati
ya ulinmzi na usalama ya wilaya ya Ikungi

Na John Mapepele, Ikungi

Mkuu wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi  leo amezindua
miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa  pamoja
baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia
ufadhiri  wa  Shirika la KOICA wa “Tuufikie usawa  wa jinsia
kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana”.

 

Mradi huo utagharimu takribani bilioni
11.5 za kitanzania  ambao
utatekelezwa  katika Wilaya ya Ikungi
mkoani Singida na Msalala mkoani  Shinyanga katika kipindi cha  miaka mitatu kuanzia sasa.

 Dk. Nchimbi amesema lengo kuu la mradi huo ni
kuchangia  katika kuwawezesha  wanawake na wasichana  kuwakwamua kiuchumi na kijamii katika mikoa ya
Singida na Shinyanga  ili kufikia usawa
wa kijinsia ambapo amewataka watendaji wote wa Serikali ambao watatekeleza
mradi huo kuwa makini katika utekelezaji wa mradi ili  malengo ya mradi huo yaweze kufikiwa.

Amesisitiza kuwa Serikali haitasita
kuwachukulia hatua kali watendaji ambao
kwa namna moja au nyingine hawataendana na kasi ya utekelezaji wa miradi
chini ya Serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema  mrai huo
ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi  ili kuwaletea wananchi  maendeleo ya
kweli.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa
KOICA  Tanzania, Bi Jieun Mo,  walengwa wasio wa moja kwa moja takribani  wakazi 40,000 kutoka kwenye wilaya  ya Ikungi na Msalala na walengwa  wa moja
kwa moja 2350 wanawake na wasichana
kutoka katika wilaya hizo watanufaika na mradi huu ambapo pia  wanaume na wanawake 6000 wa Wilaya  ya Ikungi watanufaika kwenye eneo la
muingiliano wa  hati za ardhi.

Mo ameainisha kuwa  shughuli za mradi katika kuwaweza wanawake  kwenye eneo la uchumi zitajikiza zaidi kwenye
kuimarisha uwezo wa wanawake  na
vijana   wakulima ili waweze kutumia  njia nzuri za kilimo na hali ya hewa katika
uzalishaji wa alizeti na kilimo cha bustani, kukuza uuzaji wa pamoja, ujuzi wa
ujasiriamali na wakala wa uchumi  wa
wanawake  na kuimarisha  usalama wa ardhi na umiliki.

Amesisiza kuwa  shughuli hizo zitatekelezeka  kupitia kuunda  vikundi vya uzalishaji wa kilimo cha bustani
kwa wanawake, kuunganisha  wanunuzi wa
vikundi  vya wakulima vya
wanawake,kusaidia ujenzi wa  ghala
kubwa  moja la alizeti na kituo cha
ukusanyaji kilomo cha bustani ili
kuboresha uuzaji wa pamoja na utunzaji baada ya kuvuna,.

 

Alisema pia watatoa  mafunzo ya
ujasiriamali na ufikiaji wa habari za kifedha na
kufuatilia ushauri wa usimamizi wa biashara na
fedha na kukuza  umiliki wa ardhi
pekee na wa pamoja  wa wanawake kupitia
utoaji wa  Hati za Haki za kimila za
Makaazi(CCROs).

Mwakilishi wa UN Women  Bi, Hodan Addou ameishukuru Serikali  ya
Tanzania  kuwa ushirikiano wake
katika kuhakikisha  kuwa mradi huu  hatimaye umeanza kutekelezwa ambapo amesema
Shirika lake  linaunga mkono juhudi za
Serikali za kumkomboa mwanamke ili kuondokana na  unyanyasaji wa kijinsia.

Bi Addou amesisitiza kuwa mradi
huo utasaidia uwezeshaji kijamii kwa kuwawezesha
wanawake kusimamia haki zao, kujenga ujuzi wa ujasiriamali wa wanawake na
wasichana kukabiliana  na unyanyasaji wa
kijinsia na kuimarisha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa
kijinsia kupitia kuanzisha na kuandaa vifaa katika madawati matatu ya  Polisi ya Jinsia na Watoto.

Aidha alisema pia wataaanzisha  vituo vitatu vya  huduma
ya dharura katika  vituo vya
wilaya, kuunda nafasi salama ya umma, kujenga uwezo  wa nambari ya msaada ya watoto kitaifa,
kuunda na kuimarisha Klabu za Wasichana na kuunda Kamati za ulinzi na ukatili
dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa
Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania  Zlatan
Milisic   ameipongeza Serikali kwa kuwa  na mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo
unaendana na malengo ya endelevu ya 2030 hususani lengo namba 5 kuhusiana kuwaendeleza
wanawake  katika nyanja mbalimbali na
kuongeza kuwa mwaka 2020 ni mwaka muhimu sana kwa kuwa tunaelekea  katika kutimiza miaka 25 ya azimio la
wanawake la Beijing.

Ameeleza kuwa  malengo endelevu ya 2030 yameeleza kuwa ili
kufikia maendeleo ya nchi kumtambua mwanamke ni jitihada muhimu sana  katika kuharakisha na kutimiza malengo yote
ya maendeleo ambapo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kufanya kazi
kwa karibu
sana  ili kuhakikisha wanawake wanakuwa chachu ya
maendeleo katika  nchi ya Tanzania.

Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Winfred amesema
kuwa uzinduzi wa mradi umelenga kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa
kijinsia  na kuimarisha usawa katika
jamii ikiwa ni pamoja na  kuimarisha
maisha ya wanawake ambapo amesisitiza kitovu cha matatizo ya kijinsia  ni wanaume na mila na desturi potofu
zinazomtazama mwanamke kwa kumdharirisha hivyo juhudi za makusudi  zinatakiwa
kufanywa za kuwaweka wanaume mbele ili kutokomeza unyanyasaji wa
kijinsia kwa wanawake.

Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo
amesisitiza kuwa kazi nzuri zinazofanywa na  Rais John Pombe Magufuli katika Nyanja
mbalimbali ndiyo zinazoyafanya  jumuiya
za kimataifa  kuunga mkono kwa kutoa  misaada
kupitia miradi mbalimbali hapa nchini.