Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi akizungumza baada ya uzinduzi wa mradi kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Zlatan Milisic |
Picha
ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na
wawakilishi wa mashrika ya umoja wa mataifa ,wadau wa maendeleo na kmati
ya ulinmzi na usalama ya wilaya ya Ikungi
Na John Mapepele, Ikungi
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi leo amezindua
miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa pamoja
baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia
ufadhiri wa Shirika la KOICA wa “Tuufikie usawa wa jinsia
kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana”.
Mradi huo utagharimu takribani bilioni
11.5 za kitanzania ambao
utatekelezwa katika Wilaya ya Ikungi
mkoani Singida na Msalala mkoani Shinyanga katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa.
Dk. Nchimbi amesema lengo kuu la mradi huo ni
kuchangia katika kuwawezesha wanawake na wasichana kuwakwamua kiuchumi na kijamii katika mikoa ya
Singida na Shinyanga ili kufikia usawa
wa kijinsia ambapo amewataka watendaji wote wa Serikali ambao watatekeleza
mradi huo kuwa makini katika utekelezaji wa mradi ili malengo ya mradi huo yaweze kufikiwa.
Amesisitiza kuwa Serikali haitasita
kuwachukulia hatua kali watendaji ambao
kwa namna moja au nyingine hawataendana na kasi ya utekelezaji wa miradi
chini ya Serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo amesema mrai huo
ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuwaletea wananchi maendeleo ya
kweli.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
KOICA Tanzania, Bi Jieun Mo, walengwa wasio wa moja kwa moja takribani wakazi 40,000 kutoka kwenye wilaya ya Ikungi na Msalala na walengwa wa moja
kwa moja 2350 wanawake na wasichana
kutoka katika wilaya hizo watanufaika na mradi huu ambapo pia wanaume na wanawake 6000 wa Wilaya ya Ikungi watanufaika kwenye eneo la
muingiliano wa hati za ardhi.
Mo ameainisha kuwa shughuli za mradi katika kuwaweza wanawake kwenye eneo la uchumi zitajikiza zaidi kwenye
kuimarisha uwezo wa wanawake na
vijana wakulima ili waweze kutumia njia nzuri za kilimo na hali ya hewa katika
uzalishaji wa alizeti na kilimo cha bustani, kukuza uuzaji wa pamoja, ujuzi wa
ujasiriamali na wakala wa uchumi wa
wanawake na kuimarisha usalama wa ardhi na umiliki.
Amesisiza kuwa shughuli hizo zitatekelezeka kupitia kuunda vikundi vya uzalishaji wa kilimo cha bustani
kwa wanawake, kuunganisha wanunuzi wa
vikundi vya wakulima vya
wanawake,kusaidia ujenzi wa ghala
kubwa moja la alizeti na kituo cha
ukusanyaji kilomo cha bustani ili
kuboresha uuzaji wa pamoja na utunzaji baada ya kuvuna,.
Alisema pia watatoa mafunzo ya
ujasiriamali na ufikiaji wa habari za kifedha na
kufuatilia ushauri wa usimamizi wa biashara na
fedha na kukuza umiliki wa ardhi
pekee na wa pamoja wa wanawake kupitia
utoaji wa Hati za Haki za kimila za
Makaazi(CCROs).
Mwakilishi wa UN Women Bi, Hodan Addou ameishukuru Serikali ya
Tanzania kuwa ushirikiano wake
katika kuhakikisha kuwa mradi huu hatimaye umeanza kutekelezwa ambapo amesema
Shirika lake linaunga mkono juhudi za
Serikali za kumkomboa mwanamke ili kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia.
Bi Addou amesisitiza kuwa mradi
huo utasaidia uwezeshaji kijamii kwa kuwawezesha
wanawake kusimamia haki zao, kujenga ujuzi wa ujasiriamali wa wanawake na
wasichana kukabiliana na unyanyasaji wa
kijinsia na kuimarisha mifumo ya kuzuia na kukabiliana na unyanyasaji wa
kijinsia kupitia kuanzisha na kuandaa vifaa katika madawati matatu ya Polisi ya Jinsia na Watoto.
Aidha alisema pia wataaanzisha vituo vitatu vya huduma
ya dharura katika vituo vya
wilaya, kuunda nafasi salama ya umma, kujenga uwezo wa nambari ya msaada ya watoto kitaifa,
kuunda na kuimarisha Klabu za Wasichana na kuunda Kamati za ulinzi na ukatili
dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa
Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Zlatan
Milisic ameipongeza Serikali kwa kuwa na mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo
unaendana na malengo ya endelevu ya 2030 hususani lengo namba 5 kuhusiana kuwaendeleza
wanawake katika nyanja mbalimbali na
kuongeza kuwa mwaka 2020 ni mwaka muhimu sana kwa kuwa tunaelekea katika kutimiza miaka 25 ya azimio la
wanawake la Beijing.
Ameeleza kuwa malengo endelevu ya 2030 yameeleza kuwa ili
kufikia maendeleo ya nchi kumtambua mwanamke ni jitihada muhimu sana katika kuharakisha na kutimiza malengo yote
ya maendeleo ambapo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuendelea kufanya kazi
kwa karibu sana ili kuhakikisha wanawake wanakuwa chachu ya
maendeleo katika nchi ya Tanzania.
Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Winfred amesema
kuwa uzinduzi wa mradi umelenga kutokomeza aina zote za unyanyasaji wa
kijinsia na kuimarisha usawa katika
jamii ikiwa ni pamoja na kuimarisha
maisha ya wanawake ambapo amesisitiza kitovu cha matatizo ya kijinsia ni wanaume na mila na desturi potofu
zinazomtazama mwanamke kwa kumdharirisha hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa
kufanywa za kuwaweka wanaume mbele ili kutokomeza unyanyasaji wa
kijinsia kwa wanawake.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Edward Mpogolo
amesisitiza kuwa kazi nzuri zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli katika Nyanja
mbalimbali ndiyo zinazoyafanya jumuiya
za kimataifa kuunga mkono kwa kutoa misaada
kupitia miradi mbalimbali hapa nchini.