………………………………………………………………………………………..
Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imetoa wachezaji wawili ambao wameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa Stars kitakachoingia kambini Oktoba 05 mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi.
Wachezaji hao ni Israel Mwenda pamoja na David Brayson na kwamba kama uongozi wa timu hiyo umepokea uteuzi huo kwa furaha kwani ni mafanikio makubwa na kwamba wachezaji hao wataenda kuisadia timu ya Taifa kufanya vizuri katika mchezo huo.
Kadhalika pia wachezaji hao kwakushirikiana na wachezaji wengine katika kikosi cha KMC FC wamekuwa na mchango mkubwa katika timu hiyo na hivyo kuiwezesha kufanya vizuri katika kichezo minne ya msimu wa ligi kuu Tanzania bara tangu ilipoanza Septemba 17 mwaka huu.
Hata hivyo ushiriki wa wachezaji hao katika timu ya Taifa Stars utawawezesha kujifunza mambo mazuri ambayo yataleta mchango mkubwa katika mchezo huo lakini pia kwa timu yao waliyotoka na hivyo kuendelea kufanya vizuri zaidi katika msimu wa ligi kuu Tanzania bara 2020/2021.
“ Tumepokea kwa ufaraha kubwa nafasi waliyopata wachezaji wetu kushiriki katika timu ya Taifa Stars, haya ni mafanikio makubwa kwani kikosi kinawachezaji wazuri na kwamba tuna amini katika msimu ujao tunaweza tukatoa wachezaji wengi zaidi ambao wataliwakilisha Taifa letu na hivyo kupata matokeo mazuri.