Mwanahabari mkongwe Bi.Edda Sanga akizungumza wakati wa Semina ya Wanahabari na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA iliyofanika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu TAWLA Wakili Tike Mwambipile akizungumza wakati wa Semina ya Wanahabari na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA iliyofanika Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia Semina iliyotolewa na TAWLA kwaajili ya kuwajengea wanahabari uelewa kuhusu haki na nafasi ya Mwanamke kwenye jamii.
**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waandishi wa habari wametakiwa kufuata kanuni na maadili ya uandishi wa habari ili kulinda haki na nafasi ya mwanamke kwenye jamii.
Ameyasema hayo leo Mwanahabari mkongwe Bi.Edda Sanga wakati wa Semina ya Wanahabari na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA iliyofanika Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika semina hiyo Bi.Edda amesema kuwa waandishi wengi wamekuwa wakiwakandamiza wanawake bila kufahamu pindi wanapokusanya habari
Aidha amewaomba kuzingatia sheria zilizopo ili kuwalinda wanahabari pia kujiheshimu pindi wanapokwenda kukusanya taarifa ili kuweza kumshawishi mhusika akupatie taarifa muhimu zinazoweza kusaidia kuaanda habari iliyokamilika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TAWLA Wakili Tike Mwambipile amesema wamekuwa wakijahidi kufanya kazi zao hasa kuhakikisha mwanamke anapata haki zake zote za msingi katika maeneo mbalimbali yanayomzunguka mwanamke.
Sambamba na hayo amesema katika miaka 30 ya ufanyaji kazi wamefanikiwa kufungua ofisi tano nchini katika kanda tofauti tofauti ambazo zimeweza kusaidia wanawake ambao wamekuwa wakinynyaswa na jamii inayowazunguka pia wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kuhusu nafasi ya mwanamke.