Huenda zikawa habari njema kwa wapenzi wa toleo la Infinix HOT, indapo tetesi hizi kama zitakuwa na ukweli wowote. Kupitia mtandao wa kijamii wa @infinixmobiletz inaashiria Infinix mbioni kuja na kitu kipya cha toleo la Infinix HOT -HOT 10.
Infinix HOT 10 kuingia sokoni mapema mwanzoni mwa mwezi huu, ikiwa na sifa zifuatazo kama vile betri lenye ujazo wa mAh 5200 na processor aina ya MediaTek Helio G70. Kwa kawaida tumezoea kuona Processor zenye speed kubwa kwenye simu zenye kubeba jina la kampuni au kuitambulisha Infinix katika soko la simu ulimwenguni kama vile ZERO 8.
Vile vile inasemekana Infinix HOT 10 kuja na kioo kipana cha inch 6.78 na kamera 4 zenye resolution ang’avu kwajili ya picha kali na halisi pasipo kujali muda wala eneo.
HOT 10 ni simu maalumu kwajili ya vijana hasa wanafunzi wenye kupenda burudani, hivyo basi swala la chaji si tatizo. Processor ya HOT 10 yenye teknolojia ya HyperEngine inaifanya HOT 10 kuwa miongoni mwa simu zenye kubeba games kubwa na kuangalia video pasipo kikomo.
Pamoja na sifa zote hizo lakini pia inasemekana HOT 10 haitatofautiana bei na matoleo ya awali ya HOT.