Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega akiongea na waandishi wa habari juu ya kongamano la wanawake wafanyabiashara aliloliandaa.
………………………………………………………..
Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanamke Mtanzania mfanyabiashara aishiye Marekani(UK) ,Gladness Katega Amewataka wanawake kujitokeza katika kongamano la wajasiliamali linalotarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 2 na 3 ili kujifunza na kujadili changamoto za kibiashara ili kuweza kupanua biashara zao na kumuinua mwanamke kiuchumi.
Aidha pia Alisema kuwa mbali na wanawake pia litakuwa na kongamano lingine ambalo litafanyika October 5 na 6 ambalo litawakutanisha wanaume na kujadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Katega alisema kongamano hilo litawasaidia wanawake wa Tanzania katika kuinuka kiuchumi na kuweza kutanua biashara zao
Alibainisha kuwa lengo lao kubwa la kufanya kongamano hili ni kuwaweka wanawake pamoja na kuona wanafanya biashara kwa pamoja na kuinuka
Alisema kuwa kongamano hilo litashirikisha wanawake hapa nchini pamoja na nchi mbalimbali ikiwemo Marekani ,Uingereza,Ghana ,Zimbabwe , Southafrika pamoja na Kenya na hasi Sasa zaidi ya wanawake 100 wameshathibitisha kishiriki
Alisema kuwa wanataka kuona mwanamke anainuka kiuchumi anatoka hatua moja anaenda hatua nyingine na anafanikiwa na pia napenda kuona wanawake wakibebana wakisaidiana ili waweze kufika mbali na kongamano hili litawasaidia kupata elimu watapata mafunzo watajadiliana namna ya kukuza biashara nakufikia Mataifa mengine
Alisema mgeni rasmi wa kongamano hili anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira huku akitaja wathamini wa kongamano hili kuwa ni Burka Coffee Logle ,Duluti garden,Mrembo safari,TTB,sunbright hotel,partner Africa Investment,na Kipina beauty saloon .
Alitoa wito kwa Kila mwanamke na mwanaume kuhuthuria ili kuweza kupata mitandao ya kibiashara nakujua namna ya upatikanaji wa masoko pamoja na kutatua changamoto ya namna ya kukuza biashara zao ,pamoja nanamna ya kufanya biashara kimataifa ukizingatia katika kipindi hichi ambacho baadhi ya nchi bado zinakabiliwa na janga la ugonjwa wa covid 19
Naye mwezeshaji wa mfunzo ya wanaume ya Kings master class kutoka nchini Kenya ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya RB, Dk.Robert Burale alisema wanaume wengi wanatunza maumivu moyoni na kushindwa kuyasemea kwa watu kuhusu hali ya maisha pamoja na changamoto ambazo wanakutana nazo Ndani ya familia kitu ambacho hufanya baadhi ya wanaume kupoteza maisha na wengine kufanya maamuzi ambayo Sio mazuri
“mwanamke anaweza akapata kitu akachukuwa sumu akanywa ,au hata akajinyonga lakini kwa mwanamme anaweza akaumizwa na kitu badala ya kufikiria kijinyonga yeye akachukuwa uamuzi wa moja kwa moja hivyo nitawaeleza namna ya kukabiliana na changamoto hiyo “alibainisha
Aliwataka wanaume kujitokeza kwa wingi katika kongamano hili ,huku aliwasisitiza wanawake kuwashauri wanaume wao kwenda katika kongamano ,kwani iwapo watajitokeza hawata jutia .