…..Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika stoo ya dawa ya Kituo cha Afya Kibaigwa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma ya kufuatilia ufanisi wa ICHF.
Wajumbe wa Timu ya Afya ya Halmashauri ya Kongwa wakimfatilia kwa makini Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma ya kufuatilia ufanisi wa ICHF Baadhi ya Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka HPSS.
Wajumbe wa Timu ya Afya ya Halmashauri ya Kongwa na watumishi wa Kituo cha Afya Kibaigwa wakimfatilia kwa makini Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma ya kufuatilia ufanisi wa ICHF
……………………………………………
Na. Majid Abdulkarim, Kongwa
Waganga Wakuu wa Halmashauri nchini wametakiwa kuimarisha utaratibu wa kufunga hesabu ya vifaa vya hospitali kila baada ta miezi mitatu ili kubaini hali ya uzima wa vifaa hivyo ili kupanga utaratibu wa matengenezo au mgawanyo mpya kulingana na mahitaji pale ambapo kunakuwa na ziada badala ya baadhi ya vituo kuwa vinapanga kufanya manunuzi wakati kuna ziada eneo lingine ndani ya Halmashauri au kuna uwezekano wa kutengeneza.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma ya kufuatilia ufanisi wa ICHF.
Aidha Dkt. Gwajima ameeleza kuwa Halmashauri hiyo ni mojawapo ya tano zenye karakana yake ya kutengeneza vifaa tiba ambayo sasa haian mtumishi mwenye sifa baada ya aliyekuwepo kuondoka. Hivyo ameagiza mali zote za karakana hiyo zitafutwe ziliko zirejeshwe tayari kwa kuifufua pia, lazima kila baada ya miezi mitatu Halmashauri zote nchini zifunge taarifa ya uhakiki na uchambuzi wa vifaa vyote vya hospitali.
Lengo ni kuimarisha udhibiti wa matunzo ya mali hizo na kutonunua mali ambazo ziada ipo au zinahitaji matengenezo madogo tu.
Hata hivyo Dkt. Gwajima ameeleza kuwa atarejea tena baada ya wiki mbili kwa ufuatiliaji ili kutoa somo nchi nzima.