WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ,akizungumza na washiriki wakati akifungua Mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ,alipokuwa akifungua Mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma
Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma,Amon Kinyunyu,akizungumza wakati wa Mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma
Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Dodoma,Amon Kinyunyu,akisisitiza jambo kwa washiriki wa Mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya KKKT Arusha Road Sacco’s Limited, Ibrahim Sumbe,akitoa taarifa wakati wa Mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiwa katika picha mbalimbali za pamoja baada ya kufungua Mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma.
………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda,amewataka wanachama wa Saccos kutumia mikopo kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa kwa ujumla na siyo vinginevyo.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 16 wa KKKT Arusha Road Saccos limited ya jijini Dodoma.
Mhe.Pinda ambaye pia ni manachama wa Sacco’s hiyo amesema,uwepo wa Sacco’s nchini umesaidia wananchi kujiongeza na kufanya shughuli za kujiongezea kipato lakini pia zimetoa ajira.
Aidha Pinda amesema kuwa kutoka mwaka 2015 Sacco’s zimeongezeka kutoka 4,206 hadi 6,178 mwaka huu lakini pia idadi ya wananchi waliojiunga na Sacco’s mbalimbali nchini ineongezeka katika kipindi hicho kutoka 676,202 hadi kufikia milioni 2.4.
Hata hivyo amesema kuwa ,mitaji,amana,akiba na hisa navyo vimeongezeka kutoka shilingi bilioni 428.8 hadi kufikia shilingi bilioni 819.
“Mchango wa Sacco’s siyo mdogo,ni chombo sahihi kinachoweza kuifikisha nchi mahali pazuri,pia Sacco’s zina nafasi kubwa na masharti nafuu tofauti na benki,tuzitumie .” amesema Mhe.Pinda
Hivyo nawaomba wanachama wa Sacco’s hii kukopa na kulipa kwa wakati ili wanachama wote waweze kupata fursa ya kukopa .
Aidha amewataka viongozi wa Dini nchini kuendelea kuliombea Taifa hasa tunapoelekea katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu.
“Viongozi wa dini waendele na moyo wa kuliombea Taifa ili kampeni ziende vizuri,na kila mmoja katika jamii atambue amani na utulivu ni mambo ya msingi sana.” Amesema Pinda
Awali Mwenyekiti wa Bodi wa Sacco’s hiyo Ibrahim Sumbe amesema Sacco’s hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanachama 89 ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu kuna wanachama 653 .
Pia amesema Sacco’s hiyo ilianza na fedha kiasi cha shilingi milioni 1.7 ambapo hadi Agosti mwaka huu ina shilingi bilioni 600.4 huku akisema madhumuni ya kuanzishwa Sacco’s hiyo ni kujiinua kiuchumi huku akieleza mikakati yao kuwa ni pamoja na kupanua huduma za kifedha na kujenga mtaji wa uhakika na kuendelea kujiinua kiuchumi .
Sumbe amesema tangu kuanzishwa kwake,Sacco’s hiyo imeshatoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 14 lakini pia imetoa mikopo ya viwanja kwa wanachama wake 172.
Sumbe amesema kuwa Sacco’s hiyo imetoa vitu mbalimbali vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni tano kwa vituo vya kulea wazee na watoto yatima pamoja na mashuka 200 kwa ajili ya hospitali ya mkoa wa Dodoma (General).