Mgombea Udiwani kata ya Mkuza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Fokasi Bundala akizungumza katika mkutano wa hadhara na baadhi ya wananchi wa eneo la kwa mathiasi wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji Maulid Bundala kushoto akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Mkuza Fokasi Bundala wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika eneo la kwa Mathiasi .
………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MGOMBEA Udiwani kata ya Mkuza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Fokasi Bundala amewaomba wananchi kumuamini na kumchagua kuongoza kata hiyo iliakamilishe miradi aliyokuwa akiieimamia katika awamu iliyopita.
Bundala aliyasema hayo jana wakati akizindua mkutano katika eneo la Kwamatiasi Halmashauri ya mji wa Kibaha.
Alisema, anaamini maendeleo hupatikani kwa ushirikiano hivyo kwakua awamu iliyopita kuna miradi iliyoibuliwa na bado haijakamilika utekelezaji wake anaomba tena kupewa nafasi ili akasimamie fedha kutoka Halmashauri za kukamilisha miradi hiyo.
Bundala pia alisema, katika awamu iliyopita Shilingi billion 5.2 zilitumika katika kata hiyo kutekeleza miradi ya mqji, Elimu, barabara na ujenzi wa Zahanati.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka aliwaomba wananchi kuchagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ambao watawaletea maendeleo .
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini Maulid Bundala aliwataka wananchi kuendelea kukiamini Chama hicho ambacho kinanadi sera inayoeleweka.
Bundala alisema, wagombea wa chama hicho ndio pekee wanakidhi kuhangaika na shida za wananchi kwani kila watakachoahidi kipo kwenye ilani ya Chama na kitatekelezwa.