Mgombea udiwani wa Kata ya Mzizima Fredrick Chiluba kushoto akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa mkutano wake wa kampeni |
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na mgombea udiwani wa kata ya Mzizima Fredrick Chiluba wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba |
Msanii Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo |
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo
Umati mkubwa wa wananchi wakifuatilia mkutano huo
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa
Jimbo hilo atahakikisha anajitahidi kuanzisha ujenzi wa hosteli kwa wanafunzi wanaosoma
shule za sekondari wanaokaa mbali ili kuwawezesha kusoma bila uwepo wa
vikwazo.
Hatua
hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule za Sekondari kukaa mbali
na maeneo ya shule hali inayopelekea kushindwa kufika kwa wakati kutokana na changamoto ya usafiri.
Ummy
aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mzizima katika uwanja
wa Gogovivu kwenye mkutano wake wa kampeni ambapo alisema suala hilo litakuwa
mwarobaini wa kuwaepusha wanafunzi kutokufika shuleni.
“Ninaamini
ujenzi wa Hostel utasaidia kupunguza changamoto ambazo zinawakabili wanafunzi
wanaosoma shule za mbali kutokana na kukosekana kwa usafiri kwa baadhi ya
maeneo wanayokwenda”Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba ataendelea pia kushirikiana nao kujenga miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyumba
vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.
“Ninafahamu
shule za msingi Mafuriko,amboni,rubawa na mleni kuna maadhibi miomdnboni sio
mizuri na madarasa hayatoshi,ninawaomba sana ..mchango wangu niliiutoa kabla
sijawa mbunge niaminini niweze kushirikiana nanyi kuboresha elimu hasa
miundombinu na kutafuta madawati kwa ajili ya wanafunzi”Alisema Ummy
“Lakini
pia sijaisahau shule ya sekondari Kiomoni nimewekeza ujenzi wa madarasa mawili
ninawaomba sana mnichague ili tuweze kuiboresha zaidi”Alisema
Hata
hivyo alisema pia atalazimika kubadilisha jina la shule ya sekondari Kiomoni
kwa sababu ni ya shule ya kata ya Mzizima hivyo watabadilisha jina liweze kuwa
shule ya sekondari Mzizima.
“Niaminini
tuweze kutatua changamoto za wanafunzi wa Rubawa,Mleni ambao wanakwenda mpaka sekondari ya kiomoni
kwa usafiri wenye changamoto na
kupelekea kushindwa kufika shuleni kwa wakati”Alisema