***********************************
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI
24,sept
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini ,Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo, anaanza kufuatilia fedha alizochangisha Rais Dkt. John Magufuli kiasi cha sh. milioni 68,935,000 zilizolenga kuboresha shule ya Msingi ya Soga.
Mwakamo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye Mkutano wa Kampeni ya kumuombea kura mgombea wa Urais Dkt. Magufuli, yeye nafasi ya Ubunge na Udiwani katani hapo Shomari Minshehe.
Alisema atasimamia ,kuona kazi hiyo ikifanana na fedha zilizochangishwa.
Anaeleza,Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia Halmashauri Kuu chini ya Mwenyekiti wake Dkt. John Magufuli, limepitisha jina lake awe mgombea Ubunge jimboni hapo, hivyo kabla ya Oktoba 28 anaanza kazi ya kufuatilia fedha alizochangisha Rais alipokuwa Soga.
“Wakati Rais Dkt. John Magufuli alipokuja hapa Soga alipokea kero ya uchakavu wa majengo ya shule, binafsi akachangia milioni 5 kisha akaanzisha harambee iliyokusanya shilingi milioni 68,935,000, naomba mwenyekiti uridhie nianze kufuatilia nione matumizi yake na ubora wa majengo,” alisema Mwakamo.
“Huu ndio utakuwa utaratibu wangu, popote pale ambapo viongozi wangu ngazi za juu watakapotoa maagizo, nitakuwa mstari wa mbele kufuatilia nione utekelezaji wake, ,” alisema Mwakamo.
Aidha mgombea huyo alibainisha,katika ilani ya chama hicho miaka mitano ijayo imeelezea kuifanyiakazi kwa vitendo migogoro inayohusiana na ardhi, huku akiwatoa hofu wakazi wa Soga kuhusiana na migongano yao ya ardhi.
Nae mgombea Udiwani Kata Soga Sgomari Minshehe alisema kuwa pindi wakazi hao wakiwachagua wagombea wanaotokana na chama hicho, wataungana kuhakikisha wanasimamia changamoto zinazowakabili.