Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa kampeni kata ya Ruaha mkoani Iringa
Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa akiomba kupewa ridhaa ya kuwa mbunge tena
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mgombea wa ubunge jimbo la Iringa
Mjini kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa amewahakikisha wapiga kura kuwa hakutakuwa na
diwani wala mbunge atakayekihama chama hicho kwa kuwa wameteu viongozi
wanaokipenda chama hicho kuliko mwaka 2015.
Akizungumza kwenye mkutano wa
kampeni katika kata ya Ruaha,Msigwa alisema kuwa baadhi ya madiwa walihamia CCM
kwa ajili ya uroho wa fedha na madaraka na walikuwa hawana nia njema ya
kuwatumikia wananchi katika kata zao.
Msigwa alisema kuwa wagombea wa
udiwani katika uchaguzi wa mwaka huu wamewateua wagombea ambao ni viongozi
kweli kweli na wenye nia njema ya kuwatumikia wananchi katika kuwaletea
maendeleo.
Msigwa aliwaomba wananchi wa kata ya
Ruaha kupigia kura mgombea wa ubunge, udiwani na urais wa CHADEMA kwa kuwa hao
ndio viongozi bora katika uchaguzi wa mwaka huu.
Aliwakumbusha wananchi wa kata ya
Ruaha kukichagua chama cha maendeleo na demokrasia (CHADEMA) kwa kuwa ndio chama
ambacho kimesaidia kuleta maendeleo yanayoonekana hivi sasa kwenye kata hiyo.
Aidha Msigwa aliwaomba wananchi
kuwapigia kura kwa wingi wagombea wa CHADEMA ngazi zote kwa kuwa chama hicho
kimejipanga vilivyo kuzilinda kura za wananchi hao zisiibiwe na wapinzani wao.
Kwa upande wake mgombea wa udiwani
kata ya Ruaha kupitia cha chama maendeleo demokrasia na maendeleo CHADEMA
Patrick Nyaulingo alisema kuwa wananchi wanapaswa kuchagua wagombea wa CHADEMA
kwa ajili ya kupata maendeleo ya uhakika