Home Siasa ZAIDI YA WANAWAKE 1,700 MKOANI IRINGA WAJITOSA KUTAFUTA KURA ZA DR JOHN...

ZAIDI YA WANAWAKE 1,700 MKOANI IRINGA WAJITOSA KUTAFUTA KURA ZA DR JOHN POMBE MAGUFULI

0

Mgeni rasmi ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama
cha mapinduzi(CCM) Telesia Mtewele akiongea na wanawake waliojitokeza kwenye kongamano hilo la kimkakati la kutafuta kura za wagombea wa CCM

Baadhi ya wanawake waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano hilo la kimkakati la kutafuta kura za wagombea wa CCM


Na
Fredy Mgunda,Iringa.

 

Zaidi
ya wanawake 1,700 mkoani Iringa wamejipanga kuhakikisha wanazitafuta kura za
mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli ili aweze
kuwa Rais wa Tanzania.

Akizungumza
kwenye kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama
cha mapinduzi(CCM) Telesia Mtewele alisema wanawake wa mkoa wa Iringa wanapaswa
kuyaeleza mambo ambayo Rais Magufuli amefanya kwa kipindi cha miaka mitano.

Alisema
kuwa Rais Dr Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu
bure,kukarabati majengo ya shule na kujenga majengo mapya mengi na amefuta
michango shuleni hivyo wanawake wa Iringa wanapaswa kumtafutia kura Dr John
pombe Magufuli.

Mtewele
aliongezea kwa kusema kuwa katika sekta ya elimu wanafunzi wa vyuo vikuu
wamekuwa wanapana mikopo kwa wakati na ndio maana kwa kipindi cha miaka mitano
hakuna maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ilivyokuwa miaka ya huko
nyuma.

Alisema
kuwa Rais Dr John pombe Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya afya kuwa
kujenga vituo vya afya zaidi ya 400,hospitali za wilaya,kuongeza bajeti ya dawa
kwenye hospitali zote,kuajili wafanyakazi wa sekta ya afya na ameboresha huduma
za upasuaji kwenye hospitali zote za rufaa hivyo wanawake wanajifungua bila
shida kama ilikuwa hapo awali.

Mtelewe
aliwaomba wanawake wa mkoa wa Iringa kutumia ushawishi wao kuhakikisha
wanampigia kura nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dr John pombe
Magufuli kwa kuwa anauwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo kuliko wagombea
wengine.

Aliwaomba
wanawake wa mkoa wa Iringa kwenda kuzitafuta kura za chama cha mapinduzi (CCM)
kuanzia udiwani,ubunge hadi urais hivyo wanawake waliohudhulia kongamano hilo
lilikuwa na lengo la kuhakikisha CCM inapata kura za kutosha kuliko vyama
vingine.

Kauli
mbiu yetu ni wanawake wa Iringa tunakwenda na Magufuli na ndio lengo la
kongamano hilo ni kuhakikisha tunatafuta kura za kutosha kuliko vyama vingine
vyote na kuendelea kushika dola kama ilivyokuwa kawaida ya chama cha mapinduzi
(CCM).

Naye
mratibu wa kongamano hilo Dr Ritta Kabati alisema kuwa mgombea wa urais wa
chama cha mapinduzi Dr John pombe Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuleta
maendeleo katika nchi hivyo wanawake wa mkoa wa Iringa wameamua kumuunga mkono
mgombea huyo.

Alisema
kuwa zaidi ya wanawake 1,700 walijitokeza kwenye kongamano hilo ambao lilifikia
lengo la kuhakikisha wanawake wa mkoa wa Iringa wanazitafuta kura za chama cha
mapinduzi kwa njia yoyote ile ili kuwapa ushindi wagombea wa CCM.

“Kongamano
hilo liliwakutanisha wanawake kutoka kwenye sekta mbalimbali kama vile
wafanyabisha,wanawake wanaouza kwenye bar,grocery,vilabuni,dini,taasisi
mbalkabati,walemavu,machinga,wakulima,walimu,madaktari n.k hivyo kongamano hilo
lilifanikiwa kugusa sekta zote”alisema Dr kabati

Dr
kabati aliwaomba wanawake wa mkoa wa Iringa waendeleee kuwaelimisha wananchi
wengi ambao wanapiga maendeleo yalifanywa na Rais Dr John pombe Magufuli ili
waweze kumpigia kura nyingi mgombea huyo ashinde kwa kishindo.

Aidha
Dr kabati alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano aliyokuwa Rais amefanikiwa
kuboresha sekta zote kwa kiasi kikubwa hivyo wanawake wa mkoa wa Iringa
wanapaswa kuzitafuta kura nyingi za mgombea huyo wa CCM.

kwa upande
wake mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu alisema
mwanamke ni nguzo kubwa katika amani ya jamii kwa kuwa mara zote amekuwa
akijishusha katika mambo mbalimbali na hivyo kuleta amani.

Msambatavangu
amesema wanawake wa Iringa wanakila sababu ya kuwachagua viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi kwa sababu katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kimewahudumia vizuri
na pia kimeonesha kutaka kuwahudumia vizuri kutokana na ilani ya chama hicho ya
mwaka 2020.