Uongozi wa chama cha Mchezo wa karate Tanzania JKA/WF-TZ Umetangaza rasmi kufanyika kwa Camp na Semina ya mafunzo ya mchezo huo (GASSHUKU 2020) itakayofanyika Ruvuma(Songea) kuanzia 04/12/2020( Ijumaa) hadi *06/12/2020(Jumapili).
Camp na Semina hiyo imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali kila mwaka baada ya mwaka jana kufanyika mkoani Morogoro,na mwaka huu mkoa wa Ruvuma itakuwa mwenyeji huku lengo kuu likiwa ni kuangalia viwango vya makarateka Nchini Tanzania.
Jerome Mhagama ambaye ni Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzani/J.K.A ,amewataka Karateka kujianda mapema kwa ajili ya Camp na Semina hiyo.