…………………………………………………………………………………
NA FARIDA SAIDY.MOROGORO
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefanikiwa kumuua Tembo alivamia katika msitu wa masista uliopo eneo la Njiro Block J na kusababisha kifo cha mtu moja alijulikana kama Long’ida Mollel.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mahusiano kwa Umma-TAWA Bw.Twaha Twaibu imesema kuwa baada ya mamlaka hiyo kupata taarifa juu ya uwepo wa tembo katika eneo hilo, mamlaka ilituma askari 6 walikwenda ajili ya kuimarisha ulinzi na kuzuia asilete madhara kwa wananchi Walio karibu na eneo hilo
Aidha ameendelea kusema baada ya TAWA na TAWILI kufika eneo la tukio Mwananchi mmoja ambaye pia ilijeruhiwa na kuuwawa na Tembo aliingia upande wa pili wa msitu huo ambako Tembo alikimbilia na kuweza kumjeruhi na kusababisha kifo chake.
Kufuatia tukio hilo Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori TAWA imesikitishwa na tukio hilo baya ambalo limesababisha mwanachi kupoteza maisha na inatoa pole kwa ndugu na familia wa mareehemu.