Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye mkutano leo Jumatatu Septemba 21, 2020. katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo wananchi wengi wamehudhuria kwenye mkutano huo wa kampeni.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-TABORA)
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tabora pamoja na wagombea ubunge wakiwa kwenye mkutano huo.
KUtoka kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Tabora mjini Emmanuel Mwakasaka, Mbunge Mteule wa jimbo a Kongwa Mh. Job Ndugai na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Komredi Wakasubi akimkaribisha mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ili kuzungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Mbunge Mteule wa jimbo a Kongwa Mh. Job Ndugai akizungumza na kumuombe kura Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo.
Mwanamuziki Harmonizer akitumbuiza kwenye mkutano huo wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Mgombea Ubunge wajimbo la Tabora mjini Bw. Emmanuel Mwakasaka akimuombea kura Rais. Dk John Pombe Magufuli na yeye mwenyewe.
Msanii Snura Mushi akitumbuiza kwenye mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionesha maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.