Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa chama hicho tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni leo Jumatatu Septemba 21, 2020. katika uwanja wa Milambo mjini Urambo mkoani Tabora kabla ya kuelekea Tabora mjini kwa mikutano mingine ya kampeni.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-URAMBO)
Mgombea Urais kupitia (CCM) Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono alipowasili kwenye uwanja wa Milambo mjini Urambo mkoani Tabora ili kuhutubia wananchi na kisha kuelekea Tabora mjini kwa mikutano yake wa kampeni leo Jumatatui Septemba 21, 2020.
Mbunge mteule wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma Ndugu Job Ndugai akimuombea kura Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni unaofanyika kwenye uwanja wa Milambo mjini Urambo leo.
Mgombea Urais kupitia (CCM) Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye uwanja wa Milambo mjini Urambo mkoani Tabora ili kuhutubia wananchi na kisha kuelekea Tabora mjini kwa mikutano yake wa kampeni leo Jumatatui Septemba 21, 2020.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole akizungumza katika mutano huo wakati akitoa ratiba katikati ni Mh. Job Ndugai Mbunge mteule wa CCM kutoka jimbo la Kongwa mkoani Dodoma na kulia ni mgombea ubunge jimbo la Urambo Mama Magreth Sitta.
Mgombea ubunge jimbo la Urambo Mama Magreth Sitta akielezea mafanikio ya utekelezaji wa ilani iliyopita na kuonesha ilani mpya ya CCM 2020/2025 katika mkutano huo.
Msanii wa muziki wa Singeli Pam D. akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM Mh. Dk. John Pombe Magufuli unaofanyika kwenye uwanja wa Milambo mjini Urambo.
Picha mbalimbali zikionesha maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Milambo mjini Urambo mkoani Tabora.
Baadhi ya wagombea udiwani wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa dini wakishiriki mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Milambo mjini Urambo.