**********************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete inapenda kuwajulisha wananchi kuwa wazipuuze taarifa zinazotolewa kupitia ukurasa wa twitteer wa mtu anayejiita Prof. Mohamed Janabi. Taarifa hizo siyo za kweli kwani hazitolewi na Prof. Janabi.
Ifahamike kwamba hadi sasa Prof. Janabi hana akaunti yoyote ya mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, Facebook, Instagram na Yoetube.
Prof. Janabi anatoa taarifa kuhusu huduma zinazotolewa na Taasisi, magonjwa ya moyo na afya kwa ujumla kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ya Taasisi ambayo ni yoetube kwa jina la Taasisi ya Moyo TV, twitter, facebook na instagram kwa jina la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Tunatoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na akaunti hiyo batili na wakikamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria. Aidha Taasisi inatoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na akaunti hiyo batili kwakuwa taarifa zinazotolewa siyo sahihi.