Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na maelfu ya Wananchi wa Kasulu mjini mkoani Kigoma katika Mkutano wa Kampeni za CCM leo Septemba 17. 2020
Mgombea Ubunge Jimbo la Kasulu mjini Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika mkutano huo wakati alipomuombea kura Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika Kasulu mjini
Baadhi ya wananchi wakishangilia wakati Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia kwenye mkutano wa Kampeni mjini Kasulu.
Maelfu ya wananchi wa Kasulu mjini wakimsikiliza Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akiwahutubia mjini Kasulu.
Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dk John Pombe Magufuli amesema serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 402 zote zinalala mkoa wa kigoma kwa ajii ya kufungua hii barabara ambayo tunataka iwe ya kimataifa.
Ili mtu anayetoka Kasulu anaetaka kwenda Tabora.. Dar es Salaam asikanyage vumbi na mtu anayetoka hapa kwenda Mwanza, Uganda asikanyage vumbi.
Rais Dk John pombe Magufuli amesema hayo wakati akijibu ombi la Mgombea ubunge wa jimbo la kasulu Prof.Joyce Ndalichako juu ya barabara kuanzia Kasulu katika mkutano wa kampemi uliofanyika mjini Kasulu akiwa njiani kwenda Kigoma mjini ambapo amesema hakuna tatizo kwani wanataka kutengeneza mji wa kasulu.
Rais Dk. Magufuli amesema “Inawezekana akichaguliwa itakuwa mara yake ya mwisho kupita katika barabara ya changarawe na atakapokuja tena wilayani napo atapita kwenye lami mpaka atakapokwenda”.
“Watu wa kigoma nilipochaguliwa kuwa Rais mliniambia hii sio barabara ya maana hapa kwetu mlitaka kutoka huku hadi mwanza kwa sababu mahitaji yenu mnachukulia mwanza nikasema hamna tatizo ndio maana sasa hii barabara tunaimaliza,tulianza na kilometa 50
tukaongeza kilometa 68 za kwenda Manyovu ili mtu akitaka kufanya biashara kwenda Burundi asipeleke vumbi apite kwenye lami,”amesema na kuongeza.
Rais Dk Magufuli amesema barabara ya kutoka Kigoma mpakani mwa Biharamulo, Nyakanazi kwenda mpaka Kakonko wameweka kandarasi wa kumalizia barabara zote hadi Kakonko.
Dkt.Magufuli amesema barabara hiyo itakuwa ni ya kimataifa na sio ya kitaifa itakayofanya wafanyabiashara kufanya biashara zao za kutoka mataifa mbalimbali kama Afrika Kusini, Zimbabwe,Zambia na kuingia Tanzania pale Tunduma,Sumbawanga,Katavi Kigoma, Mutukura Uganda mpaka Sudan Kusini
Mbali na barabara wanaendelea na ujenzi wa barabara zinazounganisha wilaya ya kasulu na wilaya nyingine ikiwemo barabara ya Kasulu na Manyovu yenye urefu kilometa 68.25,barabara ya Kibangu Kasulu kilomita 63 na barabara ya Ubungo kasulu yenye kilomita 59.35.
“Tumechelewa siku nyingi na ndio maana nimeyasema haya,nilipoingia madarakani nilikuwa na challenge kubwa ilikuwa ninamna gani nitaweza kuinua mkoa wa kigoma katika Maendeleo ya kweli na ndio maana lengo langu kubwa ni kuhakikisha mkoa wa Kigoma unainuka” Amesema Rais Dk. Magufuli.