………………………………………………………………………..
Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula amewaambia wananchi wa Kata ya Kahama kuwa bilioni 12 zimetengwa mwaka wa fedha ujao kuhakikisha kwamba maeneo yote ya Jimbo la Ilemela hasa yale maeneo ambayo yalikuwa hayapati umeme wa Tanesco wanapata umeme.
Hivyo amewaomba wana Kahama na Jimbo zima la Ilemela kukipigia kura na kuchagua wagombea wanaotokana na CCM ili waweze kushinda katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka ili kiweze kushinda kuanzia nafasi ya Rais,Ubunge na Udiwani ili waweze kutekeleza hayo na kuletea wananchi maendeleo.
Akizungumza wakati wa mkutano wake wa kampeni wa kuomba kura kwa wananchi uliofanyika Kata ya Kahama,Dkt.Angeline amewaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani bajeti zimeisha tengwa na hakuna mtu atakaye rukwa na kukosa umeme na awamu hiyo ya REA wote wanaenda kupata umeme.
“Tuna mitaa 171 kati ya hiyo 56 ilikua haina umeme hiyo ndio inayowekewa umeme sasa wa REA, Maendeleo yana changamoto na faida zake Jimbo la Ilemela sasa lipo ndani ya Manispaa kwa utaratibu wa kawaida hatukustahili kupata umeme wa REA, Lakini Dkt.Magufuli ambaye ni Rais wa wanyonge aliamua kuhakikisha hata mitaa iliomo kwenye Manispaa na Majiji inawekewa umeme ili mradi kila mmoja apate, niwaombe muwe na subira kwa sababu bajeti zimetengwa hakuna atakaye rukwa,” amesema Dkt.Angeline.
Pia amesema,kama hiyo haitoshi kwenye bajeti ndogo ya Tanesco zaidi ya bilioni 1 zinaenda kutatua changamoto ya umeme ikiwemo Kata ya Shibula na Sangabuye,hivyo hakuna atakaekosa nishati hiyo.
Aidha ameongoza kuwa,takribani bilioni 3.1 zimetumika kuhakikisha umeme umefika katika maeneo yote na ambao hawajafikiwa mpango upo mezani kwa Meneja wa Tanesco na ambao hawajafikiwa watapata bila shida yoyote ambapo kazi inaendelea kwa baadhi ya mitaa ya kata hiyo ikiwemo mtaa Buyombe.
Sanjari na hayo Dkt Mabula amesema kuwa changamoto ya maji katika kata hiyo itaenda kuwa historia kwani kuna mradi wa bilioni 17 unaojengwa na kampuni ya China Civil Engineering Cooperation eneo la mlima wa kwa Mkuu wa Wilaya na mkandarasi yupo eneo la kazi teyari
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela Aziza Isimbula, amesema mwaka 2015 walitoa ahadi mbalimbali ambapo wamefanikiwa kuzitekeleza hivyo wanaomba ridhaa kwa mara nyingine ili waweze kutekeleza yale yalio kwenye ilani ambayo imebeba matarajio na matamanio ya wananchi pia chama hicho kiba Mipango na dira ya kuwatumikia na kuwaletea wananchi maendeleo.