Home Mchanganyiko PROF.MCHEMBE AZINDUA KITAMBULISHO CHA WAKAGUZI WA DAWA,VIFAA TIBA JIJINI MWANZA

PROF.MCHEMBE AZINDUA KITAMBULISHO CHA WAKAGUZI WA DAWA,VIFAA TIBA JIJINI MWANZA

0

………………………………………………………………………….

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe azindua kitambulisho cha wakaguzi wa dawa, vifaa tiba na vutendanishi katika hafla ya uzinduzi iliyoenda sambamba na mafunzo ya wakaguzi hao.

Uzinduzi huo ambao umefanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wa Kanda ya Ziwa, jijini Mwanza ulihudhuriwa na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Menejimenti, Wakaguzi toka TMDA na Halmashauri mbalimbali.

Prof. Mchembe amewataka wakaguzi kuzingatia macdill yao ya kazi katika kutekeleza majukumu yao ya kiudhibiti kwani bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi ni bidhaa zinazohitaji umakini mkubwa na zisiposimamiwa vizuri madhara yake ni makubwa kwa jamii.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Bw. Adam Fimbo wakati akieleza maelezo juu ya uzinduzi huo alisema kuwa uzinduzi huo unafanyika kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika katika kuhakikisha kitambulisho hicho kinawekewa alama za kiusalama ambazo zimeunganishwa na mfumo wa taarifa za wakaguzi wa Mamlaka ambapo kadish hiyo itawezesha kubaini wakaguzi feki.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Afya kwa TMDA, Bw. Erick Shitindi, alimhakimishia KM ( Afya) kuwa Bodi itaendelea kusimamia ipasavyo utendaji wa TMDA kwa mujibu wa taratibu ili kulinda Afya ya Jamii