Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi akifungua semina ya siku tatu kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management).
Baadhi ya washiriki kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) wakiwa kwenye semina kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management).
Washiriki wakimsikiliza Dkt. Magandi katika semina hiyo.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Dickson Austin akifafanua jambo kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi.
Mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili akijibu swali kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management).
Washiriki wakiendelea kufuatilia semina kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management).
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye semina ya Usimizi wa Vihatarishi.
……………………………………………………………………….
Na John Stephen
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeandaa semina ya siku tatu kwa wafanyakazi ili kuwapatia mafunzo kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management) na namna ya kudhibiti vihatarishi wakati wa utekelezaji wa mikakati ya miaka mitano ya hospitali.
Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo watumishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) kuhusu Usimamizi wa Vihatarishi katika maeneo yao ya kazi, kupunguza vihatarishi na ikiwezekana kuviondoa ili kutoa huduma bora ya matibabu kwa wagonjwa.
Akizungumza katika semina hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management) wa Muhimbili, Bi. Pendo Chiragi katika amesema watumishi wamepatiwa mafunzo kuhusu makundi manne ya vihatarishi ambayo ni mikakati ya kupunguza au kundoa vihatarishi, kubaini vihatarishi wakati wutekelezaji wa shughuli mbalimbali, kudhibiti fedha ili itumike kama Serikali ilivyoagiza na kuzingatia sera wakati wa utekelezaji wa majukumu mbalimbali.
“Tumeandaa semina hii ili kuwajengea uwezo wataalamu mbalimbali waweze kupunguza au kuondoa kabisa vihatarishi katika maeneo yao ya kazi, lakini pia wazingatie sera, miongozo ya Serikali na maagizo ya Serikali katika matumizi ya fedha za umma,” amesema Bi. Chiragi.
Akitoa mada kwenye semina hiyo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Dickson Austin amesema Usimamizi wa Vihatarishi utawawezesha wataalamu hao kufanya kazi kwa ufanisi, taratibu na kuzingatia sera.
“Wataalamu wakifuata mfumo wa Usimamizi wa Vihatarishi (Risk Management) moja kwa moja hospitali itapata faida kwani huduma bora zitaendelea kutolewa kwa wagonjwa,” amesema Bw. Austin.
Naye Mkuu wa Idara ya Mipango na Maendeleo ya Kibiashara katika Hospitali ya Muhimbili, Bi. Jenipha Rutale amesema kazi ya idara hiyo ni kuratibu mipango mikakati ya hospitali, kufuatilia utendaji kazi, kufuatilia vihatarishi na kuratibu rasilimali katika hospitali hiyo